Habari Muhimu Kwa kila Mtanzania

Habari Muhimu Kwa kila Mtanzania

Mwiba

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2007
Posts
7,607
Reaction score
1,760
Inatakiwa kila Mtanzania afahamu ya kuwa Chama Cha CCM kimeshindwa kuongoza nchi kwa uadilifu na Mwenyezi Mungu hamfichi mnafiki ,kama wewe ni muumini wa dini ufahamu wa msemo huo utaufahamu pengine zaidi yangu.

CCM au niseme miCCM ilikuwa inatudanganya kwa muda wa miaka mingi sana ,wakidai ni viongozi waadilifu na wanaongoza bila ya kujali dini au rangi na wote ni wasafi katika ngazi ya uongozi ,lakini Mwenyezi Mungu amewaumbua mchana kweupe,amewaweka uwanjani na kila mtu mwenye akili timamu ,itabidi apambanue na aone amependwa na kuwekewewa siri ya maneno matamu ya miccm mbele ya akili na macho na masikio yake aone apime na aamue.

Wewe kama una akili ikiwa umeshaonyeshwa ubaya wa dhulma iliyofanywa na viongozi wakuu katika Taifa hili halafu ikawa bado unawakumbatia na kuwasifu na kuwatetea ,adhabu kuu itapokuja ujue hutaachwa na itakupata wewe na kukuumiza zaidi kuliko shida zilizopo sasa. Chukua uamuzi wa uhakika kwa kuikataa CCM moja kwa moja na muhimu ni kuiepuka kabisa usishirikiane nao.

Inatakiwa ujue aibu hii ilioikumba CCM si uhodari wa mtu yeyote yule bali hizi ni baraka kwako wewe Mtanzania ,ujue kuwa wakati wa kubadili nguo umefika ,una uhuru mkuu na mpana kabisa wa kuchagua nguo nyengine ,iwe inakupendeza au haikupendezi lakini nguo mpya ni mpya.

Tumia kura yako kama wewe ni mpiga kura ubadilishe upepo ,tubadilishe upepo ,usiwe mjinga usie na uelewa na kufika kujitoa fahamu na kujivalisha fahamu za upumbavu wakati Taifa linaangamia.

Leo tumepata kuyajua yaliyonyuma ya pazia la Uccm si vyema ukarudi na kubaki hukohuko CCM kama vile lililotokea si lolote si chochote ,unatakiwa upime kwa vizuri na utulize bongo lako,Miccm imetawala tokea uhuru hadi leo hakuna asiejua nini watoto wa kimaskini wanvyosota kwenye dongo,wazazi wanavyopata matatizo mahospitali,shida zisizomalizika za umeme na maji kodi inapandishwa ,umefika wakati ukitumia usitumie inakujia bili nono ,kichwa kinazunguuka ukiiona na unaambiwa uilipe,makodi yasiyo na kichwa wala miguu tunafukuzana na maaskari wa kukusanya kodi kama tupo utumwani ,michango mikubwamikubwa ya kuisaidia serikali ,wale wanaosababisha sisi kutoa michango ndio hao hao wanaozigeukia kodi tunazozitoa na kuzila ,utawala gani huu wa uwongo na ulaghai wa maneno.

Kama wewe bado una kadi ya ccm basi ichane kama huwezi kuirudisha na kama huwezi kufanya yote basi irudishe kwenye kabati uisahau humohumo,

Na kama wewe ni kiongozi mzalendo iwe mbunge au kiongozi yeyote yule ndani ya CCM basi kikimbie hicho chama na jiunge na vyama vingine vyama vipo tele na nafasi nyingi za kujazwa ili uungane na wengine.

Kwa wapiga kura wawe wastahamilivu na wanapopiga kura basi wainyime ccm kura kwani kura ni siri wala usikubali kutishwa kuwa utajulikana ,hakuna mwenye uwezo wa kukujua na hata akikujua atakufanya nini ?
 
inauma kuona Mali za umma zinaotesha parabola za watu, na hakuna mshtuko kabisa watz tunamatizo lukuki hospital shida ndio maana wao wanapeleka tez dume ughaibun!
 
Kajiandikishe leo kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa leo,msibaki hapa leo then vibibi vya ccm vimejiandkisha nyie mko busy na jf.uchaguzi ukija mnKuwa hamna sifa.
 
Ngoja tuangalie kuwa wataorubuniwa kwa chaguzi zijazo niakina nani!
 
Hakuna mbadala wa C.C, M wewe .....

Hapo zamani za kale kulikuwa hakuna m'badala wa CCM lakini kwa sasa utakuwa unajaza maji kwenye pakacha ,kwanza unatakiwa ufahamu CCM imepoteza uhalali wa kuwa Chama tawala ,kwani viongozi karibia wote wa SERIKALI YA TANZANIA ni watuhumiwa waliothibitika kuwa ni wala rushwa ,nchi haiwezi kupata maendeleo ikiwa viongozi wa juu ni wala rushwa ,kubaki madarakani ni kutumia ubabe tu na si vinginevyo ,ugunduzi wa ESCREW peke yake ilitakiwa Raisi ajiuzulu na aitishe uchaguzi ,unajua hakuna siri katika kindumbwendumbwe hiki Cha Escrow ,mbali ya kuwa mengine yamesitiriwa,lakini pazia lenye matundu halisitiri kitu ,wala mkia wa mbuzi haufichi utupu wake.

Kuanzia Raisi Waziri Mkuu na mtiririko mzima wa Serikali umepoteza muelekeo na haufai kabisa kuwepo madarakani ,sikubali kuwa Raisi tulienae hafahamu kinachoendelea,wala hajui kuwa serikali yake na ya chama chake imeashaanguka ,kinachoonekana ni watu hawa kuwapima nguvu raia na kusikiliza ,na iwe hivyo ,nitamuona au nitaiona serikali hii kama ni Nabii Suleiman ambae alikufa kitambo akiwa kwenye kiti chake cha enzi huku ameegemea bakora yake,mpaka ile bakora ilipoliwa na mchwa ndipo watawaliwa walipozinduka kuwa Mtawala alikwisha kufa kitambo.

Kwa wakati wa leo ,Raisi asisubiri nchi itokee vurugu ni vizuri kabisa akajitahidi na kuchukua jukumu kwa hicho kilichositiriwa ,wala asione kuwa anashinikizwa,hapana,ni uungwana tu ndio unaohitajika ,na wananchi walio wengi wamehabarika ,Kinana na Nape ni miccm wakipita huko mitaani wakisema waliothibitika wachukuliwe hatua ,tuseme walikuwa wanaota na wanasema kwa kubahatisha ,hapana ,ukweli ulikwishadhihirika na kuinusuru SERIKALI na Chama Chao waliona ni heri hao waliobahatika na kukamatwa na mkia wa ng'ombe ndio wezi wawajibishwe ,ili waendelee na kampeni zao ,lakini hadi leo kimya ,unafikiri wakirudi mitaani wataeleweka ? Kubaki kukaa kimya ni kuwajengea mazingira magumu wanaoitetea serikali na chama chake.

Vyama vya upinzani havitakaa kimya tayari Zanzibar wanaanza kuipiga ngoma kwa maandamano ya kutaka hadi Pinda (Waziri mkuu) awajibishwe ,ieleweke tu kuna msemo kuwa ngoma ikipigwa Zanzibar walio maziwa makuu huicheza na mshindo wa ngoma hii ni tofauti na ngoma nyingine huenda watakaoicheza wakasema hata Raisi aondoke.
 
Back
Top Bottom