H.PYLOR

H.PYLOR

Joined
Apr 6, 2024
Posts
17
Reaction score
24
# Michubuko tumboni bila H. pylori

Michubuko (Erosions au Gastritis) kwenye kuta za tumbo inaweza kutokea hata bila kuwepo kwa H. pylori.

Sababu kuu ni:-

Matumizi ya dawa mbalimbali za maumivu– (kama aspirin, diclofenac, ibuprofen) ambazo hupunguza ulinzi wa kuta za tumbo.

Matumizi ya pombe kupita kiasi kwani huchoma kuta za tumbo na kusababisha vidonda vidogo kwenye kuta za utumbo.

Msongo wa mawazo (stress gastritis) pia ni chanzo cha kuongeza asidi na kuharibu ulinzi wa tumboni.

Lishe isiyo bora kama kutumia vyakula vyenye pilipili, mafuta mengi au vyakula vya kukaanga pia ni sababu changizi .

Magonjwa mengine kama mfano Crohn’s disease au matatizo ya kinga mwilini.

# Gesi Reflux (GERD) inaweza kusababisha changamoto hii?

kwa njia mbili tofauti:
●Gastroesophageal Reflux Disease (GERD) ni pale asidi ya tumbo inapopanda juu kwenye koo/umio na mara nyingi huathiri umio zaidi kuliko tumbo lakini kwa muda mrefu reflux iliokithiri inaweza pia kuathiri tumbo na kusababisha gastritis au michubuko kwenye utumbo.

●Pia mtu mwenye changamoto ya reflux mara nyingi hupata asidi nyingi tumboni (hyperacidity) na jambo hili linaweza kuongeza uwezekano wa michubuko kwenye kuta za tumbo.

# Dalili za michubuko tumboni (bila H. pylori)
●Maumivu ya tumbo (hasa baada ya kula dawa au pombe).
●Kichefuchefu, kutapika.
●Maumivu ya kifua / kuchoma (kwa walio na reflux).
●Hamu ya kula kupungua.
●Wakati mwingine damu kwenye matapishi au kinyesi cheusi.

🩺 Tiba

Matibabu hutegemea chanzo:

Iwapo ni kutokana na dawa za kupunguza maumivu ni kusitisha hizp dawa au kubadilisha kwa ushauri wa daktari.

Kudhibiti asidi ya tumboni.
●Kupata dawa stahiki kusaidia changamoto husika.

●Dawa za kulinda kuta za tumbo
●Marekebisho ya mtindo wa maisha
●Epuka unyaji wa pombe na uvutaji wa sigara kupita kiasi
●Usile chakula kingi usiku kabla ya kulala.
●Epuka vyakula vya kukaanga, pilipili na vyakula vyenye tindikali.
●Fanya uchunguzi ikiwa dalili ni za muda mrefu kama endoscopy inapendekezwa ili kuona hali halisi ya kuta za utumbo.

📌 Kwa ufupi:
Michubuko tumboni inaweza kutokea bila H. pylori.

Reflux inaweza kuwa sehemu ya sababu hasa kwa watu wenye asidi nyingi tumboni.
R.J.Counselling&Medical Consultant
+255 692 689 788,whatsapp/Sms/Call
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom