Guys be like "Nina kazi nzuri, Gari, Nyumba, Pesa lakini sipati Mke"

Heaven Sent

JF-Expert Member
Sep 27, 2013
32,586
97,885
Mmh nimekuwa mchangiaji mzuri sana wa threads za wengine ila leo limenigusa so nimeamua tu na mimi nianzishe kathread kangu lol. Excuse my gazeti

For a while nimekuwa nikisikia na kuona wakaka wengi, especially wale ambao wanataka kuoa wakilalamika "nina gari, nina nyumba, kazi nzuri, hela etc. But sipati mke wa kuoa". Jana tu I was talking to a certain brod na yeye akaniambia the same thing. Yani hiyo statement huwa inanipa a series of unanswered questions.

Najua hiyo type na humu ndani wapo kibao. Siwatukani ila najiuliza tu, hivi mnavyowazaga hivyo huwa mnakuwa kwenye akili zenu timamu au? Tangu lini gari likaoa mke, unataka mke au unataka dereva/abiria? Una nyumba..so what exactly are you looking for; a tenant, a house keeper or what? Aliyewaambia kwamba kuwa na gari, kazi na nyumba ndo kigezo tosha cha kuoa ni nani? Hivi hukai hukajiuliza mbona nina hivyo vyote but huu ni mwaka wa 3, 4, 5 natafuta "mke" na Sijapata? Kuna tatizo gani? Ungekuwa umekaa kwa kina ukajiuliza hivyo basi naamini akili yako ingekuwa imefunguka hata kidogo.

Apart from nyumba, kazi, gari.. what else can you offer?. Kama hivyo ndo vingekuwa the only vigezo, basi kila mwenye navyo angekuwa ameoa warembo wa kutosha sana tu. Hivyo mnavyoviona ndo vigezo tosha, baadhi yetu tunaviona kama "bonus" tu kwa mwanaume anayejitambua.

Mnatiana tu ujinga humu, Tafuta pesa, utang'oa mademu wa kila aina, nachokagaaa mimi mmh. Of coz utang'oa mademu wasiojitambua, sio wanawake wenye akili zao timamu unless una extra things to offer. Kila mtu anapenda pesa/gari, lakini sio kila mtu anashobokea pesa/gari. Hivi seriously unampata msichana eti kwa sababu una gari, hivi hii century kuna watu still wanashoboka na magari, unless wana matatizo. Gari ambalo unapewa lift mara moja kwa wiki/ mwezi siku zingine zote unashika bomba, ndo limfanye mtu avue tei tei?

Hivi ukiwa na mwenye gari na wewe unakuwa unaown hiyo gari au ownership yake ni sexually transfered? Wewe utakayemla huyo girl na huyo girl wote mna matatizo tena makubwa tu. Tafuta hela zako, jitambue then utapata wanawake wanaojitambua. Wanaume malimbukeni wa hela hatuwataki. Kuna watu hata watokee kwenye Forbes na WB waseme watafinance harusi yenu, hukubali kuolewa naye ng'oooo maana hajitambui.

Mtu hana cha maana anachoongea ila kujibrag tu, nina hiki, nina kile mweee yani hapo mwenyewe anaona kashamaliza mchezo. So disgusting, ndo maturity ya mtu anayetaka kuoa huyo pyeee. Huna cha maana cha kukudefine apart from gari na nyumba mmmh. Usipendwe na mtu, basi ushajistukia "au kisa nina gari" mwee jamaniii. Siku ukimiliki jet si ndo hata humu Ukipewa like utahisi "ashasikia nina jet, ananishobokea" hahahah

Afu nyie average joes ndo mnasumbua kweli. Mtu akifanikiwa tu kidogo anajikuta Bakhresa na yeye, hivyo vigezo sasa "huyu demu sio wa hadhi yangu". Wewe hadhi yako ni ipi haswa?. It reaches a stage mnatuita watoto wa watu "scrapers" hivi una uwezo wa kuumba hata kidole wewe? If you can afford someone expensive please just go for her, sie wenye sura na shape za wajomba zetu tuacheni kwa heshima tu.

Have you ever asked yourselves watu wenye hela za uhakika, mawaziri, the high profile Men wake zao wakoje? Unakuta ni mabinti wa kawaida tu wengi, but wana class. Hata kama ukikuta binti ni famous, beautiful ana status etc, lazima "ANAJITAMBUA" kwanza. Ila nyie ndugu zangu sasa ukiwa na hela tu kinachokuja ni "a very beautiful girl" washkaji wakukomeeee. please kabla beauty haijaja pima anajitambuaje.

Uzuri, hela, status ni "BONUS" jamani. Angalia ni Vitu gani mtu anavyo vya kusustain ndoa yenu. (Sijasema muoe wanawake mvutoless, sio sifa na hata hao mvutoless sometimes wanapretend kuwa decent ili kujiongezea marks. Beauty + brain+ character). Mnajikuta mnajenga mahusiano yanayobase kwenye hela za mawazo, kesho na kesho kutwa umetetereka kidogo mke kakukimbia utamlaumu? She was there for money, hela imeisha afanye nini sasa.

Oooh nina gari, sawa utaoa "dereva/abiria " na sio "mke mwema". Kesho ukiwa huna gari usishangae dereva/abiria wako akikutoroka. Abaki kufanyaje kwa mfano, acha akatafute gari lingine

Embu leo hii, ufahamu wako utanuke kidogo. Jiulize unataka mahusiano Yenye misingi ipi, na hiyo misingi yako itakupelekea kuwa na ndoa ya aina gani. Una kitu gani cha kuoffer mahusiano yako ili yawe sustainable (things that are looking for long term sustainability) apart from vigezo "bonus".

Jitafute wewe binafsi, jijenge vizuri then jikabidhi kwa Mungu akuongoze kwenye huo mchakato. Usichague kwa macho ya kibinadamu na akili tu za kawaida. Muombe Mungu akupe macho ya rohoni, utaona hadi na attributes zisizoonekana kwa macho ya kawaida. Hela ni za muhimu sana lakini sio kitu pekee kwenye mahusiano. I pray wote mnaotafuta wake mpate wake wema eeh, mtuletee testimonies nzuri nzuri jamani

Anyway zilikuwa tu ni akili zangu za wakati huu, I'm still entitled to my opinions. Additions + Polite criticisms are warmly welcome, I don't invite insults abegooooo

HAPPY WOMEN'S DAY
 
WHAT A MSG FROM A HEAVENLY SENT YOUNG TANZANIAN LADY .....
I DO HOPE YOU ARE LEFT WITH SOME ENERGIES IN YOUR BICEPS TO HIT HARDER THE LAST NAIL TO COFFIN BEFORE WE CARRY IT TO THE GRAVE YARDS
" WHAT ARE THOSE THINGS/PARAMETERS THAT YOU GIRLS/LADIES AND WOMEN AT LARGE LOOKS TO A MAN OTHER THAN CARS, HOUSES/MANSIONS HANDSOME PAYING JOBS AND BLAHHBLAAHH THAT ALL THE DUDES YOU MEET ONCE WERE BLUFFING.????"

KIFUPI MUNAHITAJI MWANAUME MUOAJI AWE NA VIGEZO GANI?...WE ARE FROM MARS YOU ARE FROM VENUS WE MET ON PLANET EARTH...TELL US MUCH ABOUT YOUR VENUS.....THANKS AGAIN.
 
Hii ni vita unatafuta na hawa binadamu....Anyway tatizo wanawake wengi siku hizi wana sifa za kuwa mahawara tu wenye sifa za kuwa wake ni wachache mno..Wengi wanakuwa na maisha ya kuiga iga tu umarekani mwingi hadi kwenye mambo ya msingi....

"Tafuta vita vyako na uvipigane kikamilifu"Mahawara Bring it on!!!
 
Umesema kweli ila kazi kubwa ni kuondoa mentality ya kitumwa most women wako nayo kuhusu wanaume wenye magari, nyumba and etc. Kiuhalisia wanaume wenye kumiliki ulivyovitaja ndio wanakimbiliwa, sasa kama wapo wanaume wanakosa wake....big sorry kwao maana it doesnt make sense kwa maisha ya kitz ambayo percentage kubwa wanawake hawapo financially independent.
 
Ni kweli jman, manyumba, magari, mahoteli, mabasi, katka kuutaft ufalme wa Mungu vitu hivo ni ziada tuuu msidhan mkisha vpta na mwanamke ndo atatulia la hasha! wengne watakuwa mcharuko mbak mnaishia kuwalaum wanwake kuwa hawaridhiki.
 
Hii ni vita unatafuta na hawa binadamu....Anyway tatizo wanawake wengi siku hizi wana sifa za kuwa mahawara tu wenye sifa za kuwa wake ni wachache mno..Wengi wanakuwa na maisha ya kuiga iga tu umarekani mwingi hadi kwenye mambo ya msingi....
90% ya wanawake wa Tz ni gold diggers tu... Na kamwe huwezi fananisha nyumba na mwanamke.. Kila mtu anaweza kumiliki mwanamke hata 10 akitaka ila sio kila mtu anaweza kumiliki nyumba..

All in All 98% ya wanawake wa JF ni gold diggers wanaopenda vitu vizuri vizuri.. Nishapiga zaidi ya 10 humu JF hawana lolote, maisha yao ni tofauti na haya wanayoandika humu..
 
Back
Top Bottom