Guaido kuitisha maandamano mengine mapya Venezuela

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,618
Reaction score
9,607
Juan Guaido, aliyejitangaza rais wa mpito wa Venezuela ametoa wito wa kufanyika kwa maandamano mapya Jumatano na Jumamosi kwa lengo la kushinikiza jeshi, linaloendelea kumtii Rais rais aliyechaguliwa Nicolas Maduro, na kuunga mkono onyo la Ulaya kwa ajili ya uchaguzi huru.

"Jumatano kuanzia saa sita hadi saa nane mchana, nchini kote Venezuela tutamiminika mitaani (...) kuomba jeshi la nchi kuunga mkono madai ya wananachi, na Jumamosi (tunatoa wito) wa kufayika kwa maandamano kubwa nchini Venezuela na kwingineko duniani kuunga mkono onyo la Umoja wa Ulaya, "amesema Juan Guaido, Spika wa bunge la venezuela, mwenye umri wa miaka 35.

Siku ya Jumamosi nchi sita za Ulaya (Uhispania, Ufaransa, Ujerumani, Uingereza, Ureno, Uholanzi) zilimpa Nicolas Maduro muda wa siku nane kuitisha uchaguzi, la sivyo zitamtambua Juan Guaido kama rais wa mpito wa Venezuela. Muda huo utatamatika siku ya Jumapili.

Tayari Marekani na nchi kadhaa za Amerika Kusini zimetangaza kuwa zinamtambuwa Juan Guaido kama rais wa mpito wa Venezuela.

Kwa upande wa kimataifa, nchi ndogo zinamuunga mkono Nicolas maduro, ikiwa ni pamoja na China, Uturuki, Mexico na Urusi.

hata hivyo Juan Guaido ameendelea kupokea uungwaji mkono.

Siku ya Alhamisi jioni alitangaza kwamba anataka kuandaa haraka uchaguzi mpya.

Hivi karibuni Waziri wa Ulinzi, Jenerali Vladimir Padrino, alionekana katika mkutano na waandishi wa habari Alhamisi wiki hii huko Caracas akizungukwa na uongozi wa jeshi katika ngazi ya juu ili kulaani "jaribio la mapinduzi" lililofanywa na spika wa Bunge.

"Ninatoa tahadhari kwa raia wa Venezuela kwamba jaribio la mapinduzi limefanywa dhidi ya taasisi za uongozi wa nchi, dhidi ya demokrasia, dhidi ya Katiba yetu, dhidi ya Rais Nicolas Maduro, rais wetu halali," alisema waziri huyo.

Awali Majenerali wanane ambao wanaongoza Majimbo muhimu ya nchi hiyo walisema bado "wanamtii" Rais Nicolas Maduro, katika ujumbe uliorushwa kwenye televisheni ya serikali.
 
Huyo dikteta ang'olewe tu alifanikiwa kubakia madarakani kupitia uchaguzi "Feki". Anaona fahari gani kukomalia madaraka ilhali wananchi hawamtaki na uchumi ameshabaka.

Zaidi ya raia milioni mbili wamekimbia masaibu aliyosababisha yeye na kama asipong'oka basi itabidi abanduliwe tu Gaddafi style.

Hata yeye akikaa akiwaza ataendeleaje kung'ang'ania madarakani huku raia wakiwa hawamtaki? Hayo mataifa yanayomdanganya akina Russia, China, Turkey sijui na Mexico hawawezi kumsaidia kiuchumi make hawana uwezo huo kwani na wenyewe ni wapigaji tu. Hawana lolote.
 
Walianza Kama hivyo hivyo Syria Na maazimio ya umoja wa mataifa wakiongozwa na marekani kuanzia 2011 Huku mataifa yote ya kiarabu yakimuunga mkono marekani Na nchi za ulaya Ila mshirika wake mkuu Russia akabadilisha wasio mtaka mpk Leo Yuko madarakani Na nchi inaelekea kutulia na Huko yanako tendeka Hyo Hakuna tofauti na Syria lkn nakuakikishia yatapita Hyo na Hakuna kutoka mtu hpo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona hawamkamati na kumtupa lupango kama kweli amefanya "jaribio la mapinduzi"?. Issue ya Venezuela ni delicate sana na siku za Maduro zinahesabika.
 
Nahuo ndio ukweli
Fikra za mtu maskini ni ndogo sana na daima anaamin kula yake ni yakupewa na sio nguvu zake.
mataifa ya ulaya yote choka tuu hawana asilimali nyingi zaid wanategemea kuibia nchi zingine wakiongozwa na us. watapiga mikwala mwisho wa siku hakuna kitu. US ameizungua Iran na anajua deficit yake ya mafuta ni kubwa anataka kuizunguka venezuela ila mataifa mengine yasije thubutu.

huko kitanuka tuu, kama mchina amewekeza vyakutosha huko awezi kubali kuingiliwa na warafi. na mambo haya hayaitaji nchi mia kukuunga mkono bali chache zenye uthubutu. Russia akisha geuza kisogo basi tena
Walianza Kama hivyo hivyo Syria Na maazimio ya umoja wa mataifa wakiongozwa na marekani kuanzia 2011 Huku mataifa yote ya kiarabu yakimuunga mkono marekani Na nchi za ulaya Ila mshirika wake mkuu Russia akabadilisha wasio mtaka mpk Leo Yuko madarakani Na nchi inaelekea kutulia na Huko yanako tendeka Hyo Hakuna tofauti na Syria lkn nakuakikishia yatapita Hyo na Hakuna kutoka mtu hpo

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Walianza Kama hivyo hivyo Syria Na maazimio ya umoja wa mataifa wakiongozwa na marekani kuanzia 2011 Huku mataifa yote ya kiarabu yakimuunga mkono marekani Na nchi za ulaya Ila mshirika wake mkuu Russia akabadilisha wasio mtaka mpk Leo Yuko madarakani Na nchi inaelekea kutulia na Huko yanako tendeka Hyo Hakuna tofauti na Syria lkn nakuakikishia yatapita Hyo na Hakuna kutoka mtu hpo

Sent using Jamii Forums mobile app
Hivi wewe kwa akili zako unafikiri Syria kuna nchi tena pale, si ni magofu tu wamebakiza.
 
Juan Guaido, aliyejitangaza rais wa mpito wa Venezuela ametoa wito wa kufanyika kwa maandamano mapya Jumatano na Jumamosi kwa lengo la kushinikiza jeshi, linaloendelea kumtii Rais rais aliyechaguliwa Nicolas Maduro, na kuunga mkono onyo la Ulaya kwa ajili ya uchaguzi huru.

"Jumatano kuanzia saa sita hadi saa nane mchana, nchini kote Venezuela tutamiminika mitaani (...) kuomba jeshi la nchi kuunga mkono madai ya wananachi, na Jumamosi (tunatoa wito) wa kufayika kwa maandamano kubwa nchini Venezuela na kwingineko duniani kuunga mkono onyo la Umoja wa Ulaya, "amesema Juan Guaido, Spika wa bunge la venezuela, mwenye umri wa miaka 35.

Siku ya Jumamosi nchi sita za Ulaya (Uhispania, Ufaransa, Ujerumani, Uingereza, Ureno, Uholanzi) zilimpa Nicolas Maduro muda wa siku nane kuitisha uchaguzi, la sivyo zitamtambua Juan Guaido kama rais wa mpito wa Venezuela. Muda huo utatamatika siku ya Jumapili.

Tayari Marekani na nchi kadhaa za Amerika Kusini zimetangaza kuwa zinamtambuwa Juan Guaido kama rais wa mpito wa Venezuela.

Kwa upande wa kimataifa, nchi ndogo zinamuunga mkono Nicolas maduro, ikiwa ni pamoja na China, Uturuki, Mexico na Urusi.

hata hivyo Juan Guaido ameendelea kupokea uungwaji mkono.

Siku ya Alhamisi jioni alitangaza kwamba anataka kuandaa haraka uchaguzi mpya.

Hivi karibuni Waziri wa Ulinzi, Jenerali Vladimir Padrino, alionekana katika mkutano na waandishi wa habari Alhamisi wiki hii huko Caracas akizungukwa na uongozi wa jeshi katika ngazi ya juu ili kulaani "jaribio la mapinduzi" lililofanywa na spika wa Bunge.

"Ninatoa tahadhari kwa raia wa Venezuela kwamba jaribio la mapinduzi limefanywa dhidi ya taasisi za uongozi wa nchi, dhidi ya demokrasia, dhidi ya Katiba yetu, dhidi ya Rais Nicolas Maduro, rais wetu halali," alisema waziri huyo.

Awali Majenerali wanane ambao wanaongoza Majimbo muhimu ya nchi hiyo walisema bado "wanamtii" Rais Nicolas Maduro, katika ujumbe uliorushwa kwenye televisheni ya serikali.
Nchi ndogo ndogo zinazomuunga mkono Rais Maduro Ni China, Urussi, Mexico....na zinginezo...umeandika mwenyewe au umeandikiwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo dikteta ang'olewe tu alifanikiwa kubakia madarakani kupitia uchaguzi "Feki". Anaona fahari gani kukomalia madaraka ilhali wananchi hawamtaki na uchumi ameshabaka.

Zaidi ya raia milioni mbili wamekimbia masaibu aliyosababisha yeye na kama asipong'oka basi itabidi abanduliwe tu Gaddafi style.

Hata yeye akikaa akiwaza ataendeleaje kung'ang'ania madarakani huku raia wakiwa hawamtaki? Hayo mataifa yanayomdanganya akina Russia, China, Turkey sijui na Mexico hawawezi kumsaidia kiuchumi make hawana uwezo huo kwani na wenyewe ni wapigaji tu. Hawana lolote.
Unaifahamu vipi Venezuela? Ni nchi ya namna gani? Na ni nini kiini cha mkanganyiko wa hayo yote?
 
Hivi wewe kwa akili zako unafikiri Syria kuna nchi tena pale, si ni magofu tu wamebakiza.
Ninacho zungumzia mm km unauwelewa na naomba nikukumbushe Kitu walivyo vamia Libya zamira ilikua kumtoa Gaddafi madarakani kupitia maazimio ya umoja wa mataifa 2011 hawakujali kuwa nchi Ingekuwa kwenye Mazingira gn Bali wao waliangalia maslah yao Na hivyo hivyo Syria zamira Kuu ilikua kumtoa Assad madarakani kupitia direct and direct war hawakujali nchi Inge kuwa Mazingira Yp bl n maslah tu waliangalia n kwl nchi imebomoka lkn km mwanzo waliweza kujenga kwa nn washindwe lkn Leo hii zile kelele za marekani Na washirika wake kuwa hawamtaki zimepungua Kutokana Na uwelewa wko MDOGO kuhusu siasa Ndio maana umeandika hivyo lkn I guarantee you and note my name pale ni km Syria tu kelele Nying na sanction tu bc lkn kutoka madarakani n Kitu kugumu Kwa sababu russia na China wameinvest pale pesa Nying wakiruhusu tu wame kula hasara n Kitu kugumu sana Na ninakushanga hutafakari kwa Kina Na km unakumbuka baada ya Libya kuvamiwa kipindi kile putin n waziri Mkuu baada Ya kuwa rais tena alizungumza hawata kubali tena kilicho Tokea Libya kitokee tena. Cold War coming soon

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona hawamkamati na kumtupa lupango kama kweli amefanya "jaribio la mapinduzi"?. Issue ya Venezuela ni delicate sana na siku za Maduro zinahesabika.
Kwa nini Maduro asumbuke naye? Guaido hana jeshi, hana mamlaka yoyote ndani ya nchi zinazomtii. Hata Polisi hawamtii. Sasa kwa nini asumbuke naye?

Venezuela ana hazina kubwa ya mafuta kuliko Saudi Arabia ambayo ni mshirika wa Marekani. Unafikiri ni kipi kitatokea kama Venezuela akiingia kwenye hilo soko la mafuta huku akikataa kuwa kibaraka wa Marekani? Umeshawahi kujiuliza uchumi wa Marekani na oil prices zina uwiano wa namna vipi?
 
Kwa nini Maduro asumbuke naye?
Maduro hamuwezi. Guaido ni Speaker na President wa National Assembly. Amequote vifungu vya Katiba yao vinavyompa uhalali wa kujitangaza, albeit kinyume na utaratibu. Kule nadhani hakuna mambo ya "Mhimili uliojichimbia chini zaidi". Angekuwa ni mtu mwingine kafanya aliyoyafanya Guaido, sasa hivi angekuwa ndani kwa treason charges
 
Back
Top Bottom