GPS tracking system kwa Bajaj

Unaongeza kama uwekavo kwenye cm vocha
Ina maana kuwa unaweza kununulia simu ambayo ipo mbali muda wa internet? Kwa mfano simu ipo Temeke na iko ON na wewe uko Kimara. Je unaweza kuongeza muda wa internet? Nauliza kwa sababu huwa situmii service ya pre-paid hivyo sio nguli wa haya mambo!
 
Kwenye maonyesho ya sabasaba mwaka huu niliona kwenye banda la VETA wakiweka hizo track kwa bodaboda, watafute utafanikiwa.
 
Ili aweze kuta-track kwa kutumia simu si ni lazima simu iwe na internet connection muda wote? Sasa kama mwizi akiiba hiyo bajaji na muda wa internet ukiisha utaongezaje? Au unaweza kuongeza remotlly?

Yes.. unaweza nunua MB remotely he has to remember namba ya simu tu, ni nzuri zaidi akatumia Halotel, na bundle ya wanavyuo, which is very cheap, unapata MB kibao eg. sh. 500 unapata 600Mb kwa wiki nzima ambazo hazitaisha, na simu iwe ndogo aifiche kwa kui design chini ya spedometer ya boda boda.. ili isionekane..!!
 
Nenda kinondoni morroco kaulizie ofisi za car track ila wao kila mwezi unalipia sina uhakika na bei ilikuwa 25elfu Kwa mwezi,au nenda sido dar kipawa kaulizie nasikia kuna ofisi inafungia wa bodaboda watakufungia
Ahsante ndugu, nimewasiliana nao gharama zao kwa mwezi ni sh. 50,000 ambayo kwangu ni gharama kubwa
 
Asante kwa ushauri mzuri
 
Hoi itasaidia hata kwa wenye boda, nisaidie jinsi ya kuagiza na zenye ubora maana wawezapata ila muda wote inataka intermet connection sasa kwa network yetu hapa nchini maeneoengi chenga
GPS au Global Position System, yenyewe huwa haihitaji Internet Connection, yenyewe huwa ina track kwa kutumia Satellite...kuna makampuni maalum huwa wanatoa hiyo huduma, unakwenda pale na bajaji yako wanakufungia vifaa vya kuweza ku track hiyo bajaji yako, na wanakwenda mbali zaidi kwa mfano ukitoa taarifa kwamba bajaji yako imeibiwa wanauwezo wa kuizima, isiwake na wakai track mpaka ilipo,.
 
Haswaaa hili ndio hitaji langu mkuu, so unaweza kunitajia baadhi ya kampuni zinazotoa huduma hii pls
 
Kwa nini siyo hapa kwenye Uzi huu ili uunufaishe na wengine... Hiyo 50,000 ni kwa mwezi au ndio malipo ya jumla


Ukidhani unachofikiri uko peke ako Sahau. Mi nilitaka kuintroduce trackr sticker ambayo kuna manajamii kaitaja. Ndio mambo ya fursa

Nina supply Trackr Bravo, Trackr stickers etc. Ukishanunua kwa 50,000 hakuna malipo ya ziada. Unaweza kuunganisha kwenye school bag ya mwanao ukajua wapi alipo. Baiskeli, bajaj, funguo nk
 
GPS device si inahitaji utaalamu kufunga ndugu au mtu yoyote anaweza kufunga? Je kuagiza toka China gharama zake ni kiasi ghani?
Ni kakifaa kadogo tu kama kifuniko cha chupa ya maji ya uhai au saa ya mkononi.
 
Ili aweze kuta-track kwa kutumia simu si ni lazima simu iwe na internet connection muda wote? Sasa kama mwizi akiiba hiyo bajaji na muda wa internet ukiisha utaongezaje? Au unaweza kuongeza remotlly?
Itakuwa sawa na kuliwa kuku na mayai yake.
 
Kwenye hiyo track R kuna mushkeli kidogo kwenye umbali. Au nimekosea mimi.

Track it down. From anywhere If an item goes missing, TrackR's Crowd GPS network will help you find it. When another user of the TrackR app comes within 100ft range of your lost item, you will receive a GPS update of where your item is

Mimi huwa natumia hii hapa chini kwenye gari na pikipiki zangu. Haina gharama kubwa baada ya kuifunga zaidi utatakiwa kuhakikisha betri haichomolewi na unaweza kuweka vocha ya 500 kwa mwezi mzima. Vicha yenyewe ni weww kuituma kama unamtumia mtu salio. Hivyo utatakiwa kujua namba ya kila gps.
 

Attachments

  • IMG_20161115_101101.jpg
    87.4 KB · Views: 65
  • IMG_20161115_101124.jpg
    105.8 KB · Views: 72
Mkuu hebu elezea tunapataje hiyo huduma hata mimi nataka kufunga kwenye vyombo vyangu vya usafiri
 
nicheki nikufungie hizo system 0714890018, www. isecure. co. tz
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…