Google Now Yatinga Kwenye iOS

ManiTek TV

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2011
Posts
410
Reaction score
159

​
Google sio wachoyo, au tuseme wanaamini kuwepo kuwa bidhaa na huduma zao kuwepo katika gajeti mbali mbali ndio mafanikio ya biashara zao. Google Now ilianza kutoka wakati toleo la awali kabisa la Android Jelly Bean 4.1 lilipotoka na Nexus 7, baada ya karibu mwaka mmoja watumiaji wa iPhone, iPad na iPod Touch nao wataweza kuwa na huduma hiyo kwenye gajeti zao.

Ingawa sio kadi zote zinapatikana katika Google Now ya iOS lakini inafanya kazi kwa ufanisi na kasi ile ile inayopatikana kwenye simu na tableti za Android. Miongoni mwa kadi zinazokosekana katika Google Now hii ni pamoja na boarding pass na pedomita ya mwezi. Kama ilivyo kwenye Android unapotaka kufunga kadi za taarifa unaweza kufanya hivyo kwa kuzipangusa (swipe) na kadi hutoweka mara moja.

​
Kwenye Google Now ya iOS huwezi kutumia kuanzisha matumizi ya kutafuta kwa sauti kwa kutumia kauli ya “Google” kwenye iOS kama ilivyo kwa watumiaji wa Google Now kwenye Android. Tofauti kubwa zaidi ni kwamba kwenye Google Now hii pia hakuna taarifa za moja kwa moja (notifications) kwa watumiaji.

Unaweza kutumia huduma nyingine za app hii kama vile kuona miadi yako (appointments), au taarifa za msongamano wa magari katika njia unayokusudia kupita, Kwa wastani Google wanaonekana kutokuwa tayari kuifany aGoogle Now ya iOS iwe sawa na ile ya Android ingawa wanajua kuwa kwa kuipeleka huduma hii kwenye vifaa hivi basi kutaongeza idadi ya watumiaji wa Google.

Ikiwa mtumiaji wa iPhone, iPad au iPod touch, ili kupata huduma hii pakua (download) au boresha (update) app ya Google na anza kuitumia kwa utulivu kabisa. Kwa kifupi watumiaji wa Android wana jambo moja pungufu la kuwaambia watumiaji wa iPhone kwamba hawana hichi, wakati gajeti za iOS zitabaki kuwa gajeti pekeez enye Siri. kwa hili matokeo ni iOS 2 - 0 Android.

Chanzo: gajetek habari

​
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…