Good bye Zaltan Ibrahimovic

isackkallindi

Member
Jan 10, 2014
25
21
MICHEZO Usitarajie kumuona tena Zlatan Ibrahimovic uwanjani kwa mwaka 2017
By Isack kalindi

Bado wachezaji na benchi zima la ufundi la Man United halitakuamini kwa kilichotokea kwa mshambuliaji wao tegemeo raia wa Sweden Zlatan Ibrahimovic kuwa hawezi kurejea uwanjani kwa siku za karibuni kufuatia jeraha lake la goti alilolipata wakati wa game ya Europa League dhidi ya Anderletch.

Kwa mujibu wa mitandao ya Ulaya hususani ESPN umeripoti kuwa Zlatan Ibrahimovic kufuatia jeraha lake la goti la kulia alilolipata atakaa nje ya uwanja hadi mwezi January 2018, kitaalam Zlatan anaumwa Anterior Cruciate Ligament (ACL), hivyo atalazimika kufanyiwa upasuaji ambao utamchukua muda mrefu kurudi uwanjani.

Jeraha hilo alilolipata Zlatan mastaa wenzake ambao wamewahi kukutana na tatizo hilo wamekuwa wakikaa nje ya uwanja kwa zaidi ya miezi 9, mfano Zouma wa Chelsea aliumia katika mchezo dhidi ya Man United 2016 lakini alilazimika kurudi uwanjani baada ya miezi 11.

Hii ni mwaka 2016 Zouma wa Chelsea alipopata jeraha kama la Zlatan lililomuweka nje ya uwanja kwa miezi 11.

Inawezekana huo ndio ukawa mwisho wa Zlatan kuvaa jezi ya Man United kutokana na mkataba wake kuripotiwa kumalizika mwisho wa msimu huu, sasa haijajulikana kama staa huyo aliongeza mkataba na Man United au alikuwa ameingia makubaliano ya awali kama hakuongeza ana asilimia ndogo ya kupewa mkataba mpya akiwa katika majeruhi na akiwa na miaka 35.
 
Aende zake tuu...kwanza score rate yake ni ndogo sana ukicompare na chance za kufunga anazozipata...pili Mourinho alikuwa anamuogopa au labda ana maslah nae ya kibinafsi,maana hata akiboronga vipi mourinho alikuwa hawezi kumpiga sub...Kuumia kwake ni advantage kwa man utd maana wakina Rashford watapata chance zaidi ya kucheza na pia next season umuhimu wa kusajili straika mpya utakuwa umeongezeka maradufu!!!
 
Naungana na wewe kwa hili,mwenyewe nilikuwa natamani kutokee sababu ya Zlatan kuwa nje kwa kipindi kirefu haswaa kwa kipindi hichi tunachoenda kumaliza ligi.

Moja ni Mou kushindwa kuacha kumpanga kutokana na sababu za kimkataba,lakini kiukweli hesabu zinamkataa,pamoja na kufunga magoli Zaidi ya 18+ lakini idadi ya Mchezo,dakika na chance anazopata haziendani na magoli aliyofunga, kwa maana nyingine Zlatan anaweza kuwa ni sababu ya Man U kuwa hapa ilipo kama mfungaji tegemewa,enzi za Ruud van now angekuwa na goli Zaidi ya 20,mana timu inazuia vizuri,kiungo cha uhakika,ushambukiaji ndio tatizo.

Kutokana na mfumo anayotumia Mou,mara nyingi hutegemea mfungaji mkuu.

Sasa nini maana yake ikiwa Ibra atakuwa inje kwa muda mrefu,Mou itabidi kucheza kama alivyocheza na Chelsea bado timu itakuwa na tatizo la ufungaji lakini inabidi kuwaruhusu Viungo nao kufanya kazi ya ushambuliaji kidogo Pogba anaweza kuwa kiungo huru na kuanza kufunga au Herera mana Matta naye yupo nje.
 
Nakuungeni mkono tena mimi naona amechelewa kuumia angeumia mapema tusingekuwa hapa mana timu nzima ilikuwa inamwangalia yeye sasa kutakuwa na balance
 
Nilisema sana kule kwenye jukwaa, watu wakanishambulia, uwezo wa zlatan wa kufunga mabao umepungua kiasi kwamba kwa maoni yangu ni bora angepewa rooney mara mia angetufikisha juu kuliko tulipo, wakaniambia nisishabikie tena untd, sifurahishwi na kuumia lakn bora akae nje, mwengine ni lingard, natamani japo apate tatizo lolote la kiafya litakalomfanya akae nje mpaka msimu umalize
 
Naungana na wewe kwa hili,mwenyewe nilikuwa natamani kutokee sababu ya Zlatan kuwa nje kwa kipindi kirefu haswaa kwa kipindi hichi tunachoenda kumaliza ligi.

Moja ni Mou kushindwa kuacha kumpanga kutokana na sababu za kimkataba,lakini kiukweli hesabu zinamkataa,pamoja na kufunga magoli Zaidi ya 18+ lakini idadi ya Mchezo,dakika na chance anazopata haziendani na magoli aliyofunga, kwa maana nyingine Zlatan anaweza kuwa ni sababu ya Man U kuwa hapa ilipo kama mfungaji tegemewa,enzi za Ruud van now angekuwa na goli Zaidi ya 20,mana timu inazuia vizuri,kiungo cha uhakika,ushambukiaji ndio tatizo.

Kutokana na mfumo anayotumia Mou,mara nyingi hutegemea mfungaji mkuu.

Sasa nini maana yake ikiwa Ibra atakuwa inje kwa muda mrefu,Mou itabidi kucheza kama alivyocheza na Chelsea bado timu itakuwa na tatizo la ufungaji lakini inabidi kuwaruhusu Viungo nao kufanya kazi ya ushambuliaji kidogo Pogba anaweza kuwa kiungo huru na kuanza kufunga au Herera mana Matta naye yupo nje.

Man u siipendi. Lakn linapokuja swala la ufundi. Huyu zlatan ni balaa pale man u kaipeleka pazuri timu, sijaona wakumfikia pale labda kwa vile white ndy maana. Ila angelikua mweusi mwenzetu kaleta mchango like zlatan naamini wengi wangejitokeza kumsifia kwa kua ni BLACK.
 
Waafrika Ndo Maana Hatusogei Kwa Mambo Mengi, Tumejawa Na Majungu, Kutokuwa Na Shukran. Kwan Rooney Wkt Timu Inazama Hakuwepo? Morinho Ni Mvumilivu Akimuamini Mtu, Alimvumilia Pogba, Hata Huyo Rooney Aliendelea Kumpa Nafasi. Msifananishe Soka La Bongo Na Ulaya, Ibra Yupo Vzr.
 
Aende zake tuu...kwanza score rate yake ni ndogo sana ukicompare na chance za kufunga anazozipata...pili Mourinho alikuwa anamuogopa au labda ana maslah nae ya kibinafsi,maana hata akiboronga vipi mourinho alikuwa hawezi kumpiga sub...Kuumia kwake ni advantage kwa man utd maana wakina Rashford watapata chance zaidi ya kucheza na pia next season umuhimu wa kusajili straika mpya utakuwa umeongezeka maradufu!!!
Mkuu sio alikuwa anamuogopa ni issue za mkataba.
 
Aende zake tuu...kwanza score rate yake ni ndogo sana ukicompare na chance za kufunga anazozipata...pili Mourinho alikuwa anamuogopa au labda ana maslah nae ya kibinafsi,maana hata akiboronga vipi mourinho alikuwa hawezi kumpiga sub...Kuumia kwake ni advantage kwa man utd maana wakina Rashford watapata chance zaidi ya kucheza na pia next season umuhimu wa kusajili straika mpya utakuwa umeongezeka maradufu!!!
Anauza Jezi tu hapo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom