Goli la mkono ni nini?

Goli la mkono ni nini?

Mtalebani

Member
Joined
Aug 22, 2014
Posts
23
Reaction score
57
Unaweza ukamwokota mbwa njiani, kisa umemwona akimbwekea mtu alotaka kumpokonya mtoto andazi.. Mbwa huyo ukaona anafaa kufuga. Ukampeleka kwako, hukujali kelele za majirani kuhusu ushenzi wa mbwa huyo...
Ukaingia buchani na kwenye machinjio, ukakusanya kwa bidii ngozi za kumlisha, ukampeleka josho, akapigwa maji freshi, ukamkabidhi lindo... Geti kuu la kuingia nyumbani kwako..

Siku ya kwanza akakulaki, kama mfalme,
Siku ya pili akakulambalamba, ukajisikia mmiliki..
Siku ya tatu akakutana na mbwa jike, akaja naye hom kwako... Ukaona, Ah! Mambo haya ni sawa, wanasaidiana ulinzi... Ukawatunza wote...
Wiki imeisha, mbwa jike katawala, kubweka yeye, na ambwekea amtakaye...hata wewe ulomlea akubwekea...

Ukamaindi... Unataka mbwa jike huyo umtose, Alaaaa! Mbwa ulomkirimu siku ya kwanza kawa kama pilipili! Hataki kupangiwa, wala hakukuomba umchukue siku ile... Yeye anataka kukaa na jike lake, ajua alikolitoa.... Hataki kukumbuka ulivyohaha machinjioni ukisaka mlo wake, mikono yako ikichafuka damu na kutobolewa na mifupa ili tu atunzike!

Unapanga siku ya kumuua huyo jike shupa, unaandaa mtega safi! Umepata steki ulonunua bei ghali, unapaka sumu fresh... Huyo! Huyo! Huyo! Waelekea hom... Ebwana! Kufika unashambuliwa wewe hadi majirani wanapiga 911... Mbwa wamekuchakaza... Mtego umekulipukia!

Haya, umekumbuka shuka wakati kumeshakucha...! Kazi ni kwako
 
Ni ushindi uliopatikana kwa njia zisizo halali
 
Hivi viroba vimeanza kuruhusiwa kuuzwa tena?
Mbona hueleweki
Hembu weka wazi watu wajue kwamba unalenga nini
 
Usijaribu kuingilia uchumba wa kiumbe chochote unaweza kupotea unataka kumngoa mke wa mbwa
 
Ni pale unapokosea timing kati ya kuvuta pin na kutupa bom, linakulipukia mkononi!!
 
Back
Top Bottom