VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,004
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Samwel Sitta amepata nafasi adimu. Jana,Samwel Sitta amenukuliwa akisema kuwa kuna viongozi waandamizi Serikalini waliofanya usanii wakati wa ujio wa Obama na kutafuna shilingi bilioni 8 za kitanzania.
Waandamizi hao walianzisha kampuni 'hewa' na kuzoa tenda zote zilizohusu yote yaliyozunguka ujio wa Obama na mkutano wa Partnership.Malalamiko ya Sitta yameshatua TAKUKURU ambao wamesema kuwa wameanza kufanya uchunguzi juu ya tuhuma hizo. Huu ni wakati wa Waziri Sitta kuachia madaraka na kupata heshima.
Ni wakati wa Sitta kujitoa Baraza la Mawaziri ili awe na muda mzuri wa kushirikiana na TAKUKURU na hatimaye mafisadi yafikishwe mbele ya sheria. Waziri Sitta asithubutu kupoteza nafasi hii adimu.Akijitoa kwa wanaolalamikiwa na kujiunga nasi tunaolalamika,ataaminika.Ataheshimika.
Atajiweka pazuri.La sivyo,Sitta atapotezwa na malalamiko yake yasiyokwisha. Atadharauliwa kama mtu 'wa kulia lia' tu. Hatabaki hata na chembe ya heshima za kulalamika. Waziri Sitta ataamua moja sasa!
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam