DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,129
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imemtangaza aliyekuwa mgombea Ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Godwin Mollel kuwa ndiye mshindi wa Ubunge wa Jimbo la Siha mkoani Kilimanjaro.
Uchaguzi huo mdogo ulifanyika jana Desemba 30, 2025 baada ya kusogezwa mbele kutokana na aliyekuwa mgombea Ubunge wa jimbo hilo kupitia Chama cha Wananchi (CUF) Daudi Ntuyehabi kufariki dunia kabla ya uchaguzi mkuu kufanyika.
Pia Soma: Mgombea ubunge CUF Siha auawa kinyama katika ugomvi
Akitangaza matokeo hayo usiku wa Desemba 30, 2025 Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo hilo, Marko Masue amesema Dkt. Mollel alipata kura 51,769 sawa na asilimia 78.4 huku mpinzani wake wa Chama cha NRA, Ntaana Thobias akipata kura 4,992 sawa na asilimia 7.56.
Naye, mgombea wa Chama cha ACT Wazalendo, Ashukuriwe Matemu alipata kura 3,678 sawa na asilimia 5.57, Mgombea wa Chama cha Sauti ya Umma (SAU), Mdoe Ambazi alipata kura 3,128 sawa na asilimia 4.74 huku mgombea wa Chama cha MAKINI, Daniel Nsila alipata kura 2,007 sawa na asilimia 3.04.
Pia Soma: INEC yasitisha Kampeni za ubunge Jimbo la Siha kufuatia kifo cha mgombea wa CUF, Daudi Ntuyehabi