Habari Wanajamvi.
Naomba kujuzwa juu ya gharama za solar power(Full Gadgets i.e Charger Controller,Panel,Battery & Inverter ) ambayo nitaweza kuwasha Tv,King'amuzi pamoja na Taa Sita.Mwenye Ufahamu Navyo Tafadhari.
Nashukuru sana wadau!!
Ila mimi nina kachumba changu kamoja sasa kwa gharama ya 1.5Mil kwa chumba kimoja ni shida aisee,labda niitafute hiyo 600,000 maana ndio nafuu angalau.
sola system ya kuendesha fridge,taa 8 pamoja,dek,fen,dicoda,tv pamoja na radio ipo andaa 3.9 ml umeme wa uhakika kwa warant ya miaka 25 chin ya uangalizi wa steps solar
Ulieuliza swali la kuongezea Fridge umesaidia wengine hapa.
Halafu naomba wengine mtujuze hii issue ya Tanesco kuingilia mradii huu,nasikia kwamba kuna charges unalipia tanesco kwa kutumia Solar power kila mwezi?hata kama sio dili lao.Mambo ya Serikali hayo.
Mfano ni huku Zanzibar,kwamba ukichimba kisima cha maji basi lazima kila mwezi ulipie Idara ya Maji.Hapo Malipo ni ya kufikrika tu,maana kila mtu analipa bei yake.
sola system ya kuendesha fridge,taa 8 pamoja,dek,fen,dicoda,tv pamoja na radio ipo andaa 3.9 ml umeme wa uhakika kwa warant ya miaka 25 chin ya uangalizi wa steps solar
nikusahihishe kwanza, umeme hutunzwa kwenye betri sio invetor kazi ya invetor ni kuubadili umeme toka kwenye dc(mkondo mnyoofi) kwenda kwenye ac(mkondo geu),endapo utawasha vifaa vyote ulivyo violozesha umeme utadumu kwa muda ule tulio ukadili mfano masaa 6 au s7,iweleke kwamba solar inategemea sana mahesabu na matumizi ya muitaji hivyo anafungiwa mteja kulingana na masaa na vifaa atakavyo viita vitategemeana