Wakuu habari!!!!!
Jana nilifanikiwa kufika gereza la Keko kumsalimia ndugu yetu Maxence Mello.
Kwanza nikifarijika sana kumkuta akiwa mwenye tabasamu la kutosha kama mtu aliye na imani na matumuaini makubwa ya kuishinda vita iliyo mbele yake. inaonesha bado ana moyo wa ushujaa wa kusimamia kile anacho kiamini.
Katika 'visiti' yangu ya jana ilikua ni mara yangu ya kwanza kufika gerezani hapo na niliona nitumie fursa hiyo kufahamu ubora wa huduma zitolewazo hapo. Binafsi niliyaon maeneo mawili ambayo nadhani ni vema yakaongeza ufanisi katik utoaji wa huduma.
1. Ukiingia katika geti kuu unakutana na askari wa ukaguzi, katika eneo hilo unpaswa uache simu kwa kuambatanisha na kitambulisho chako vyote vinafungwa kwa pamoja ili iwe rahisi kukufahamu mara utakapo rudi kuchukua, lakini katika huduma hiyo changamoto niliyo iona ni kuwa unapoa acha simu yako hakuna sehemu unaandikisha jina lako kwamba umeacha simu yako pale japo kwenye daftari, hatari ya hii iko pande zote mbili ni rahisi askari kukataa kwamba uliacha simu yako pale maana hakuna uthibitisho wowote kwamba simu yako ilibaki pale, au vile vile raia anaweza kuja kudai simu hata kama hakuiacha maana hauna orodha ya watu walioachiwa simu..
2. Pale keko kin huduma ya duka ambapo mara nyingi watu wanao watembelea ndugu zao hununua pale zawadi za kuwapelekea, lakini cha kushangaza hawatoi receipt za EFD taasisi kama hii ya serikali ilipaswa kuwa mfano bora wa utoaji wa receipt hizi, nimeona taasisi nyingine kama za jeshi wakito risit hizi sijajua kama magereza kwa wao sio lazima au hawajaamua kufanya hivyo.
Rai yangu kwa uongozi wa gereza hili ni kuwa iongeze ufanisi zaidi katika utoaji wa huduma..
[HASHTAG]#freemaxencemello[/HASHTAG].
Nawasilisha