Gereza la Keko liongeze Umakini na Ufanisi katika utoaji wa huduma

tashwishwi

JF-Expert Member
Sep 25, 2014
2,095
2,000
Wakuu habari!!!!!

Jana nilifanikiwa kufika gereza la Keko kumsalimia ndugu yetu Maxence Mello.
Kwanza nikifarijika sana kumkuta akiwa mwenye tabasamu la kutosha kama mtu aliye na imani na matumuaini makubwa ya kuishinda vita iliyo mbele yake. inaonesha bado ana moyo wa ushujaa wa kusimamia kile anacho kiamini.

Katika 'visiti' yangu ya jana ilikua ni mara yangu ya kwanza kufika gerezani hapo na niliona nitumie fursa hiyo kufahamu ubora wa huduma zitolewazo hapo. Binafsi niliyaon maeneo mawili ambayo nadhani ni vema yakaongeza ufanisi katik utoaji wa huduma.

1. Ukiingia katika geti kuu unakutana na askari wa ukaguzi, katika eneo hilo unpaswa uache simu kwa kuambatanisha na kitambulisho chako vyote vinafungwa kwa pamoja ili iwe rahisi kukufahamu mara utakapo rudi kuchukua, lakini katika huduma hiyo changamoto niliyo iona ni kuwa unapoa acha simu yako hakuna sehemu unaandikisha jina lako kwamba umeacha simu yako pale japo kwenye daftari, hatari ya hii iko pande zote mbili ni rahisi askari kukataa kwamba uliacha simu yako pale maana hakuna uthibitisho wowote kwamba simu yako ilibaki pale, au vile vile raia anaweza kuja kudai simu hata kama hakuiacha maana hauna orodha ya watu walioachiwa simu..

2. Pale keko kin huduma ya duka ambapo mara nyingi watu wanao watembelea ndugu zao hununua pale zawadi za kuwapelekea, lakini cha kushangaza hawatoi receipt za EFD taasisi kama hii ya serikali ilipaswa kuwa mfano bora wa utoaji wa receipt hizi, nimeona taasisi nyingine kama za jeshi wakito risit hizi sijajua kama magereza kwa wao sio lazima au hawajaamua kufanya hivyo.

Rai yangu kwa uongozi wa gereza hili ni kuwa iongeze ufanisi zaidi katika utoaji wa huduma..

[HASHTAG]#freemaxencemello[/HASHTAG].

Nawasilisha
 
Puyet Babel

JF-Expert Member
Aug 29, 2013
3,594
2,000
Sijaelewa hapo kwenye duka la kununua zawadi!

Kumbe mtu akiwa amefungwa magereza hupelekewa zawadi
anyway nawapongeza wote mliofika keko magereza kumfariji CEO wa JF

#FreemaxenceMello#
 
Humphnicky

JF-Expert Member
Dec 1, 2010
1,999
2,000
[HASHTAG]#freemaxencemelo[/HASHTAG]
[HASHTAG]#justiceforlema[/HASHTAG]
[HASHTAG]#wewantbackalivebensaanane[/HASHTAG]
 
Habibu B. Anga

Verified Member
May 7, 2013
6,656
2,000
Ukilinganisha na magereza mengine Keko wana afadhali kubwa sana..

Kwanza nimependa mfumo wao baada ya kusikia unaonana ana kwa ana na uliyeenda kumuona..

Magereza mengine wanaweka dirisha la wavu au kioo kati kati..

Kuhusu hayo mapungufu mengine madogo madogo nadhani yanarekebishika!

Tatizo la kuandikisha simu ni kwamba, utatakiwa uandike modeli ya simu na details ya kuitofautisha..
Yani mfano umeacha simu ya Samsung, hautaandika Samsung tu, bali utaandika Samsung, S6, rangi yake, n.k nadhani mlolongo unakuwa mrefu sana ndio maana wanarahisisha kwa kuifunga na kitambulisho chako..

Magereza mengine wamerahisisha zaidi! Kabla hujamuona ndugu yako wanakuamuru tu uzime simu! Sasa wewe jitoe ufahamu ukaiwashe ukiwa unaongea na ndugu yako alafu wakugundue hahahaha utaelewa vile virungu vina kazi gani..

# FreeMaxenceMelo
 
MLAU

JF-Expert Member
Aug 23, 2007
4,727
2,000
Hongera kwa kufika Keko,hayo uliyoyaona hasa kuacha vitu vyako kwa askari bila kurekodi ni kawaida na hakuna anayepoteza kitu ila ushauri wako ni mzuri pia.wala hakuna wa kudai wakati hakuacha kitu.Hiyo ni miaka nenda rudi iko hivyo.

Na kuna MTU alikuwa anahamasisha watu humu JF waende Keko kwa wingi sana mpaka Serikali ishtuke nikamuonya asijaribu kuhamasisha kitu cha hivyo.

Mbona yeye mwenyewe mpaka Leo kimya ina maana hajaenda kumuona Melo?

Melo will be free very soon
 
tashwishwi

JF-Expert Member
Sep 25, 2014
2,095
2,000
Sijaelewa hapo kwenye duka la kununua zawadi!

Kumbe mtu akiwa amefungwa magereza hupelekewa zawadi
anyway nawapongeza wote mliofika keko magereza kumfariji CEO wa JF

#FreemaxenceMello#
Mkuu unaweza kununua hata juice ya kumpelekea mfungwa/mahabusu, mbona ni kawaida hiyo
 
tashwishwi

JF-Expert Member
Sep 25, 2014
2,095
2,000
Ukilinganisha na magereza mengine Keko wana afadhali kubwa sana..

Kwanza nimependa mfumo wao baada ya kusikia unaonana ana kwa ana na uliyeenda kumuona..

Magereza mengine wanaweka dirisha la wavu au kioo kati kati..

Kuhusu hayo mapungufu mengine madogo madogo nadhani yanarekebishika!

Tatizo la kuandikisha simu ni kwamba, utatakiwa uandike modeli ya simu na details ya kuitofautisha..
Yani mfano umeacha simu ya Samsung, hautaandika Samsung tu, bali utaandika Samsung, S6, rangi yake, n.k nadhani mlolongo unakuwa mrefu sana ndio maana wanarahisisha kwa kuifunga na kitambulisho chako..

Magereza mengine wamerahisisha zaidi! Kabla hujamuona ndugu yako wanakuamuru tu uzime simu! Sasa wewe jitoe ufahamu ukaiwashe ukiwa unaongea na ndugu yako alafu wakugundue hahahaha utaelewa vile virungu vina kazi gani..

# FreeMaxenceMelo
Mkuu kwa sababu pia sina experience na magereza mengine, hongera zao
 
Mr.Junior

JF-Expert Member
Sep 8, 2013
10,287
2,000
.jpg
Wakuu habari!!!!!

Jana nilifanikiwa kufika gereza la Keko kumsalimia ndugu yetu Maxence Mello.
Kwanza nikifarijika sana kumkuta akiwa mwenye tabasamu la kutosha kama mtu aliye na imani na matumuaini makubwa ya kuishinda vita iliyo mbele yake. inaonesha bado ana moyo wa ushujaa wa kusimamia kile anacho kiamini.

Katika 'visiti' yangu ya jana ilikua ni mara yangu ya kwanza kufika gerezani hapo na niliona nitumie fursa hiyo kufahamu ubora wa huduma zitolewazo hapo. Binafsi niliyaon maeneo mawili ambayo nadhani ni vema yakaongeza ufanisi katik utoaji wa huduma.

1. Ukiingia katika geti kuu unakutana na askari wa ukaguzi, katika eneo hilo unpaswa uache simu kwa kuambatanisha na kitambulisho chako vyote vinafungwa kwa pamoja ili iwe rahisi kukufahamu mara utakapo rudi kuchukua, lakini katika huduma hiyo changamoto niliyo iona ni kuwa unapoa acha simu yako hakuna sehemu unaandikisha jina lako kwamba umeacha simu yako pale japo kwenye daftari, hatari ya hii iko pande zote mbili ni rahisi askari kukataa kwamba uliacha simu yako pale maana hakuna uthibitisho wowote kwamba simu yako ilibaki pale, au vile vile raia anaweza kuja kudai simu hata kama hakuiacha maana hauna orodha ya watu walioachiwa simu..

2. Pale keko kin huduma ya duka ambapo mara nyingi watu wanao watembelea ndugu zao hununua pale zawadi za kuwapelekea, lakini cha kushangaza hawatoi receipt za EFD taasisi kama hii ya serikali ilipaswa kuwa mfano bora wa utoaji wa receipt hizi, nimeona taasisi nyingine kama za jeshi wakito risit hizi sijajua kama magereza kwa wao sio lazima au hawajaamua kufanya hivyo.

Rai yangu kwa uongozi wa gereza hili ni kuwa iongeze ufanisi zaidi katika utoaji wa huduma..

[HASHTAG]#freemaxencemello[/HASHTAG].

Nawasilisha
.jpg
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom