George Iron Mosenye katika ubora wake. Jamaa kwa ujumbe huu anafaa kuwa Katibu Mkuu wa mabaharia Tanzania

MR KUO

JF-Expert Member
Jan 8, 2016
2,433
3,318
HABARI za asubuhi marafiki! Ni siku ya jumanne ya tarehe nne…. Na hakuna kingine ukishaona maandishi haya asubuhi basi ni kipengele adhimu na bora kabisa cha YA-WALIMWENGU.

Leo nina haraka sana, ngoja niwapeleke moja kwa moja katika chakula chetu cha leo.

Na leo nipo kuwachambua wanaume linapokuja suala la mahusiano, kuna mambo huwa yanajirudia na kuna mengine ni mageni. Hivyo weka utulivu nikueleze yanaweza kukukwamua hata ukatoka katika huo u-bachela.

________________
TWENDEE!
__________________

Zaidi ya nusu ya wanaume hubadili mashuka yao ile siku ya kwanza kutembelewa vyumbani na wachumba/wapenzi wao kwa siku ya kwanza. Yaani hii nd’o ile siku ya kila mwanaume kujifanya hapendi uchafu… ila sasa mzoeane uje kama mara nne hivi… ndo utajua kuwa hujui!

Wanaume wengi hufikiria kuwa ni heri mwanamke awe na sura nzuri na mwili mbaya kuliko kuwa na sura mbaya kisha mwili mzuri. Kiukweli ofisi ni reception bwana, pakiwa pa hovyo basi kuna uwezekano huko ndani ni hovyo zaidi.

Asilimia kubwa ya wanaume wanaweza kujihusisha katika mapenzi na wanawake ambao wana umri mkubwa lakini asilimia tisini wakiulizwa hukataa kata kata kuwa hawezi kufanya kitu kama hicho. Nd’o walivyo hawa mabaharia, usiyaamini sana majibu yao.

Robotatu ya wanaume wote huhifadhi namba za wasichana walioachana nao bila kuzifuta kabisa. Wasichana hufuta namba za wanaume punde baada ya kuachana. Si unaona sasa wanaume walivyo na mioyo ya upendo wa dhati… sisi ni wazee wa matumaini kuwa ipo siku tutarudiana.

Wanaume huamini kuwa KAZINI na SHULENI ndizo sehemu sahihi kabisa za kupata msichana wa kujihusisha naye kimapenzi.

Asilimia 40 ya wasichana wapo radhi kumkatalia mwanaume kuwa nao katika mahusiano ikiwa tu rafiki yake hajampenda!!! Ona sasa hawa viumbe, yaani nd’o maana unaambiwa kama umempenda mwanamke, hakikisha kwanza marafiki zake wanakukubali… yaani hawa huwa wana vikao vyao vya kutuchambua. Unakuta mwanamke wako hana maamuzi juu ya mahusiano yake, anaamuriwa na marafiki.

SISI HATUNA MAMBO MENGI YAANI! Humchukua mwanaume dakika kumi na tano tu kumsamehe mwanamke na kuendelea naye kuwa katika mahusiano!!... Na tukisamehe ndo tumesamehe, sema machungu tutalipizia kwa kutoka na rafiki yako.

MSIJE KUSEMA SIKUWAAMBIA! Kutokana na tafiti, siku ya JUMATANO imeonekana kuwa siku ambayo mahusiano mengi mapya huzaliwa!! Jumatano ni kesho, kama kuna mtu unataka kumtongoza leo, ahirisha… nenda kesho ukachukua mzigo wako. Nakuhakikishia atakukubalia, akikataa nipigie simu nimuweke sawa.

PUNGUFU YA HAPA WEWE TUNAKUHITISHIA KIKAO. Mwanaume wa kawaida kabisa kwa siku huona wanawake watano ambao anatamani wangekuwa wake zake!! EEh! Yaani kuna siku unamuona binti wa kazi pale home ndo alifaa kuwa mkeo kabisa, hujakaa sawa baamedi unasema huyu sasa ndo wa kuoa…. Hakikisha wanafika watano kwa siku tafadhali….

HII NI KWA WOTE SASA! Ukiwa unabishana na mpenzi wako ikafikia hatua moyo wako ukawa unapiga mara mia moja kwa dakika basi hautaweza tena kumsikia mwenza wako anachosema!! Na hapa ndo pabaya, panaposababisha ugomvi mkubwa unaoweza kuhatarisha maisha. Maana kila mmoja hasikii tena mwenzake anasema nini…..

WAZEE WA KUPASHA VIPORO MPOO! Asilimia kumi ya wanaume wanaotalikiana na wake zao hujikuta wakiingia katika mahusiano na wanawake ambao zamani waliwahi kuwa nao katika mahusiano!! Huwa tunaacha akiba sisi…. Hatupendi kuanza upya.

NGUVU YA PESA KATIKA MAPENZI. Unaambiwa kuwa Kati ya mahusiano kumi yanayoanzia kazini manne kati ya hayo huishia kuwa ndoa!!! Jiongeze hapa hii haiji kibahati, hapa mwanaume anaamini kapata mwanamke wa kusaidiana naye, na mwanamke anajiona ameangukia mikono salama kiuchumi. Ila wenzangu na mimi sasa wa ninasikilizia michongo…. Kupata ndoa huwa kazi sana.

TUCHEKE TU JAPO NDO UKWELI! Katika mahusiano yanayoanzia mitandao ya kijamii ambapo wawili hawajaonana. Kila mmoja huwa ana lake la kuhofia ambapo, MWANAMKE huhofia sana kukutana na mwanaume muuaji… wakati MWANAUME huhofia kukutana na mwanamke mnene. Daaaah!! Mbona mimi napenda wanene, kwani wenzangu wanene waliwakosea nini hadi muhofie kiasi hicho??

Wataalamu wa mahusiano wanasema kuwa msichana akikupatia namba yake na kisha akaacha kupokea simu zako wala kujibu meseji zako basi havutiwi na wewe!! Hapa unataka nikushauri nini sasa, ACHA USUMBUFU Ndugu!

ZINGATIENI HILI! Utafiti unaonyesha kuwa mwanaume hujionyesha wazi kuwa yu penzini baada ya kukutana na mpenzi wake mara nne tu lakini mwanamke hujionyesha yu penzini mpaka akutane na mwanaume mara 14. Kwa hiyo ukikutana na msichana ile siku ya kwanza anasema amekufa ameoza juu yako, simama mkamate ucharaze hata makofi manne. Akiuliza nini shida, mwambie mlimwengu nimesema aache uongo!

Wanamahusiano wa kwanza hubusiana wanapokutana mara ya pili, Sio siku ile ya kwanza!! Kama wewe siku ya kwanza tu, tayari ushamgeia mate mwenzako nyie ni WAHUNI TU! Keshokutwa mtaachana!

Ukikutana na msichana kwa mara ya kwanza na akalipia huduma zote mlizotumia basi ujue kuwa hakuja kuonana nawe kwa nia ya mapenzi!!! Usije ukajiongeza kiboya sasa ukasema Yes! Kanipenda mwenyewe, huyu amekusaidia maisha tu! Haujapendwa….

MWANAUME USIFANYE HAYA! Makosa makubwa ambayo wanaume huyafanya wanapokutana na msichana kwa mara ya kwanza yanayosababisha kupuuzwa ni haya!! 1. Kuchelewa eneo la tukio, 2. kujisifia sana, 3. kumtaja sana msichana ambaye mliachana. Sasa kama hili la tatu nd’o kosa kubwa mnooo, Braza hata kama alikuwa anakata viuno kama feni, wewe kausha usilete stori zake hapo sio pahali sahihi.

LIJUE HILI! Wanapokutana wanaume wanne ama zaidi huzungumza juu ya michezo ama siasa… lakini wanapokutana wanawake wanne ama zaidi huzungumza juu ya WANAUME. Huwa wanajua kuchambua sana wanaume hawa…. Wewe hadi ukubaliwe ujue kuna kamati zimekutana mnooo!

LA MWISHO HILI HAPA NA NINA UHAKIKA NALO 100%. Tafiti zinaonyesha kuwa wanawake huvutiwa zaidi na wanaume wakiwa wamevaa nguo za BLUU!! Yaani hako kapicha kangu hapo chini nina kasuti kangu ka bluu, bwana bwana! Hiyo siku walitaka kuniua, huyu kanibusu, huyu kanishika mkono kaniachia namba ya simu, huyu anataka anipe lifti kwenye gari lake, mwingine ananiambia ofisini kwao kuna nafasi ya kazi atanifanyia mpango nipate, mwingine anasema yeye anachotaka nizae naye tu! Atalea mwenyewe…… aisee hii suti sijawahi kuivaa tena maishani mwangu. Sitaki kesi mimi! Na sitaki tena nguo za bluu….. hii siku wangeniua wale wanawake!

Majina yangu ni George Iron Mosenya (Mlimwengu)
Whatsapp: 0655 727325.

Nakutakia wakati mwema, endelea kumtegemea Mungu katika yote yaliyo mbele yako. Usichoke!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom