Gazeti la Mwananchi na upotoshi kuhusu mfumo wa kanda wa CHADEMA

Dec 11, 2010
3,321
6,328
Leo gazeti la Mwananchi kwenye habari yao yenye kichwa "Mkakati wa Chadema kuingia Ikulu" wameandika...

Dar es Salaam. Siku moja baada ya katibu mkuu wa Chadema, Dk Willbrod Slaa kuwataka Watanzania wajiandae kwa "Serikali Mpya" aliyodai itapatikana Oktoba 31 baada ya Uchaguzi Mkuu, gazeti la Mwananchi limebaini mkakati wa ushindi unaopangwa na chama hicho cha upinzani.

Hadi sasa, Chadema ndio chama kinachoongoza kwa upande wa upinzani kulingana na matokeo ya Uchaguzi Mkuu uliopita na wa Serikali za Mitaa uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana, na inaonekana kujipanga kupaka mafanikio makubwa zaidi mwezi Oktoba.

Katika Uchaguzi Mkuu wa 2010, mgombea wa CCM, Jakaya Kikwete alishinda kwa kupata asilimia 61.17, ikiwa ni pungufu ya asilimia 20 ya kura alizopata mwaka 2005, wakati Chadema ilimsimamisha Dk Willbroad Slaa aliyepata asilimia 26.34 akiwa anasimama kwa mara ya kwanza.

Huku CCM ikiwa katika mchakato mgumu wa kumpata mrithi wa Kikwete uliogubikwa na adhabu dhidi ya makada wanaotajwa kutaka nafasi hiyo, Chadema iliweka mkakati wake katika kikao cha Kamati Kuu kilichofanyika Januari mwaka huu.

Kwa mujibu wa habari ambazo Mwananchi imezipata, chama hicho kimelenga pamoja na mambo mengine kupeleka madaraka kwenye ngazi ya kanda badala ya mambo yote kutegemewa yafanywe na makao makuu.

Chadema, habari hizo zinasema, imeunda kanda 10 ambazo ni Kanda ya Serengeti, inayoundwa na mikoa ya Simiyu, Shinyanga na Mara, Ziwa Victoria (Geita, Mwanza, Kagera), Nyanda za Juu Kusini (Rukwa, Mbeya, Njombe, Ruvuma, Iringa), Kanda ya Kusini (Lindi na Mtwara).

Nyingine ni Kanda ya Kati (Singida, Dodoma na Morogoro), Kanda ya Kaskazini (Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara), Kanda ya Magharibi (Tabora, Katavi na Kigoma), Kanda ya Pwani (Temeke, Ilala na Kinondoni), Kanda ya Unguja(Kusini Unguja, Kaskazini Unguja na Mjini ) na Kanda ya Pemba (Kusini Pemba na Kaskazini Pemba).

Kanda hizo zitawezeshwa kwa mafunzo na kiuchumi ili kuzijengea uwezo wa kushughulikia mambo yake, hasa wakati wa uchaguzi bila ya kutegemea ofisi kuu.

Kwa mujibu wa habari hizo, kanda hizo pia zinazindua vikundi vyake vya ulinzi, ambavyo kazi kubwa inaonekana itakuwa ya kulinda kura ili kukabiliana na tatizo kubwa la upungufu wa rasilimali watu wakati wa Uchaguzi Mkuu.

Pia kuundwa kwa Mabaraza ya Uongozi ya Kanda kutawezesha mashauri mengi kwenye ngazi ya mikoa kutatuliwa bila ya kutegemea ofisi kuu.

Tayari mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe ameshafanya ziara kwenye baadhi ya kanda na kufanya vikao na Mabaraza ya Uongozi ya Kanda kuyashirikisha mikakati hiyo, sambamba na kuzindua vikundi vya ulinzi.

Lakini alipoulizwa kuhusu mpango huo, Mbowe hakutaka kuwa bayana.

"Sasa nikiweka wazi mikakati yetu, si itakuwa kama nimewauzia wengine. Hapana siwezi kuiweka wazi ila tunajipanga kuelekea Uchaguzi Mkuu," alisema Mbowe, ambaye pia aligombea urais mwaka 2005 wakati Kikwete akiingia Ikulu kwa mara ya kwanza.

Lakini mtu aliye karibu na uongozi huo wa Chadema alikiri kuwapo kwa mkakati huo.

"Unajua mkakati huo unakwenda sambamba na kutoa mafunzo kwa viongozi mbalimbali wa chama kuanzia ngazi ya chini kabisa," alisema akiomba jina lake lisitiriwe.

"Tunataka kanda hizi ziwe na uwezo wa kupambana na si kusubiri kila jambo kutoka makao makuu." Taarifa zaidi zinaeleza kuwa ziara hizo za Mbowe pia zinalenga kufanya maboresho ya kiutendaji ikiwa ni pamoja na viongozi wa chama hicho kupewa mafunzo maalum na mbinu mbalimbali. "Chama kimebaini kuwa ili kushinda, hakiwezi kupambana na adui kutoka sehemu moja tu, ni lazima kiwe nchi nzima.

Hilo tumeliona katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa," alisema mtoaji habari huyo. "Kinachofanywa sasa ni kuhakikisha kuwa kila kanda inakuwa na nguvu ya kufanya mambo yake yenyewe.

Yaani kila kanda itaweka mkakati wake wa kukiimarisha chama na kukabiliana na misukosuko yote ya kisiasa. Makao makuu ya chama yatakuwa yakitoa maelekezo tu." Jumamosi iliyopita, Dk Slaa alisema katika mkutano wa hadhara uliofanyika Isaka wilayani Kahama kuwa nchi haina budi kujiandaa kwa serikali mpya.

Alisema Chadema itashika nchi kwa kuwa wananchi wamechoshwa na serikali iliyopo sasa ya CCM, kwamba ili kuongeza nguvu za kuking'oa chama hicho kikongwe, wananchi wanapaswa kuunga mkono juhudi za Ukawa.

Dk Slaa, ambaye aliwahi kuwa mbunge wa Karatu kabla ya kugombea urais mwaka 2010, anatazamiwa kuteuliwa tena na chama chake kuwania urais na ni mmoja wa watu wanaopewa nafasi kubwa ya kupitishwa na Ukawa kupeperusha bendera ya upinzani dhidi ya mgombea wa CCM, kwenye mbio za Ikulu.

Mbali na kufanya vizuri mwaka 2010, Chadema ilipiga hatua kubwa zaidi kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana baada ya kunyakua viti vingi vilivyokuwa vinashikiliwa na CCM na vyama vingine vya upinzani.

Chadema ilifanya vyema zaidi katika Kanda ya Serengeti kwa kupata kura nyingi katika vijiji, vitongoji na mitaa, kura ambazo hazijafikiwa na kanda yoyote.

Kanda nyingine zilizofuatia kwa kufanya vizuri katika uchaguzi huo ni Kanda ya Ziwa Victoria na Kanda za Kaskazini.
==================

Ukweli kuhusu kanda na mambo matano ambayo mwananchi wamepotosha.

1. Uundwaji na mfumo wa kanda ulipitishwa na baraza kuu la Jan 2013, nia ikiwa kugatua madaraka (decentralization) kwenda kwenye kanda. Na kimsingi hizi kanda ni kuiishi sera yetu ya majimbo ya 2005 na kama inavyoelekezwa na katiba ya chama ibara ya 7.6, wao Mwananchi wameongelea kanda kwa jicho la uchaguzi wa mwaka huu na si kama mfumo rasmi wa kukiendesha chama kwa sasa ambao umetambuliwa na katiba.

2. Mwananchi wanasema "...kuundwa mabaraza ya uongozi wa kanda kutawezesha..." ukweli ni kwamba mabaraza ya uongozi yalikuwepo since day one kanda zilipozinduliwa/undwa, mabaraza ya uongozi kwenye kanda wajumbe wake ni wenyeviti na makatibu wa mikoa, na wilaya/majimbo. Viongozi hao tayari walikuwepo walialikwa tu kuja kuhudhuria kikao chao husika.

3. Mwananchi wanaandika "...kila kanda itaweka mkakati wake..." si kweli kwamba kila kanda itakuwa na mkakati wake, bali tuliweka maazimio mahususi na maazimio ya jumla kwenye kanda. Kila kanda haiwezi kuwa na mkakati wake maana mikakati yote inaratibiwa ikiwa na maelekezo na taarifa mfanano.

4. Vikosi vya ulinzi viko kikatiba na vimeelezewa bayana kuwa "... Ni chombo cha ulinzi na usalama wa mali na maslahi ya chama na viongozi...", si kweli kwamba vikosi hivyo vimeundwa kwa ajali ya uchaguzi. Ni vikosi ambavyo tunavyo kikatiba tangu kuandikwa upya kwa katiba ya chama toleo 2006.

5. Imeandikwa "...mkakati wa kanda unaendana na kutoa mafunzo..." swala la mafunzo kwenye chama ndio kiupambele chetu na kama tungetafuta takwimu za mafunzo kwenye vyama vya siasa sisi tunaongoza kwa kuwa na program mbalimbli za mafunzo, mafunzo yamekuwa yanatolewa kwa viongozi mbalimbali hata kabla ya mfumo wa kanda. Kwa mfano wadau wetu na marafiki wanaofadhiri mafunzo ndani ya chama (KAS) wameanza ushirika na sisi tangu 2004 kabla hata ya kuanzishwa kwa mfumo wa kanda, kanda zimeanza Jan, 2013.

Wakatabahu.

Kanyawana Shemng'ombe Mtoi Mohamedi.
 
Yule jamaa aliyeingia kimkakati pale d.msyaki si ndiye mhariri aliye mfukuzisha tido?
-hii ya chadema ana leta kadabra zisizo mantiki wala mashiko,maana ukweli hujisimamia daima na unafik hulegalega na kusahaulika milele!
*poor mwananchi!*
 
ukweli utabaki palepale hata ukanushe. Mifumo yenu ya kuleta vurugu kupitia vikundi vya ulinzi visivyo na busara lazima yawekwe wazi na mtaumbuka sana,huu mwanzo tu.

uliona wapi RB wanaleta vurugu kama siyo na wewe unaongea kiunazi tuu!
-green guard walipompiga mbunge rose kamili mbona ulishangilia,leo cdm wanatekeleza matakwa ya katiba yao ambayo hata msajili anayo mnaanza kulalamika?
*mwaka huu kuelekea ushindi wa ajabu october 2015 kila mtumikavna c.c.m atakuwa amesema kila uongo anao uona utamwingizia pato toka c.c.m!
 
Kamanda Mtoi Tuna Wandishi wengi sana Makanja kwenye hii Taluma yetu.. Namakanjanja wengi ni wale wanaochukua bahasha kutoka kwenye kale ka ukoo wa Fisi

Mwanahabari Huru
 
Magazeti yanatumika vibaya sana kwenye siasa za CCM! Wanajaribu kila hali kutapatapa lakini hawawezi!

Hakuna hila ambayo itafanikiwa!
 
Ukweli utabaki palepale hata ukanushe. Mifumo yenu ya kuleta vurugu kupitia vikundi vya ulinzi visivyo na busara lazima yawekwe wazi na mtaumbuka sana,huu mwanzo tu.

Na Green Guard nawo ni kikundi cha aina gani?
 
Nilisoma gazeti la mwananchi kwa makini lakini sikuelewa kumbe ulikuwa upotoshaji mkubwa hawa waandishi wa habari wanatumiwa na ccm kupotosha
 
Ondoa wendawa.zimu wako hapa. Ni lini CHADEMA walishawahi kuleta fujo? Uwe mkweli na utoe mifano sahihi vinginevyo, jianglie sana sisi wengine hatupendi ujing kwenye masuala ya maisha ya watu.

Green guard wanafanyaga nini? wako kwa mujibu wa katiba ipi inayotambuliwa kisheria? Utekaji na utesaji ambao wamekuwa wakifanya hata mbele ya polisi, umeidhinishwa na nani?

Mbona roho yako ni kama ya joka vile? Wewe ungeikuwa na chembe ya Utu , usingediriki kufanya kazi ya fitna hapa kuwasingizia red brigade kufanya vurugu ambazo hawajawahi kufanya. Leta ushahidi la sivyo uache upum.bavu. Ukiendelea, shauri lako.

Ukweli utabaki palepale hata ukanushe. Mifumo yenu ya kuleta vurugu kupitia vikundi vya ulinzi visivyo na busara lazima yawekwe wazi na mtaumbuka sana,huu mwanzo tu.
 
Chadema wanapenda Ukanda sana.

Bahati mbaya hujui kuwa CCM pamoja na kubeza sana mfumo wa kanda wa chadema nao wameanzisha kimya kimya tena kwa aibu ya chumbani mfumo wa kanda 12. Wanaona aibu kutoka front na kusema wameanzisha mfumo wa kanda kama CHADEMA
 
Bahati mbaya hujui kuwa CCM pamoja na kubeza sana mfumo wa kanda wa chadema nao wameanzisha kimya kimya tena kwa aibu ya chumbani mfumo wa kanda 12. Wanaona aibu kutoka front na kusema wameanzisha mfumo wa kanda kama CHADEMA
Ccm kila kitu wana copy naku paste toka Chadema alafu wanasimama nakusema wongo
 
Ondoa wendawa.zimu wako hapa. Ni lini CHADEMA walishawahi kuleta fujo? Uwe mkweli na utoe mifano sahihi vinginevyo, jianglie sana sisi wengine hatupendi ujing kwenye masuala ya maisha ya watu. Green guard wanafanyaga nini? wako kwa mujibu wa katiba ipi inayotambuliwa kisheria? Utekaji na utesaji ambao wamekuwa wakifanya hata mbele ya polisi, umeidhinishwa na nani? Mbona roho yako ni kama ya joka vile? Wewe ungeikuwa na chembe ya Utu , usingediriki kufanya kazi ya fitna hapa kuwasingizia red brigade kufanya vurugu ambazo hawajawahi kufanya. Leta ushahidi la sivyo uache upum.bavu. Ukiendelea, shauri lako.
jamaa mjinga kweli wewe,badala ya kujenga hoja unakuja na vitisho kwa mtu mzima,jinga wewe. Juzi tu hapa RB wamemtesa mlinzi wa babu yenu matukio mengi tu,njoo kwa hoja vitisho sio hoja kubwa zima wewe.
 
Nilisoma gazeti la mwananchi kwa makini lakini sikuelewa kumbe ulikuwa upotoshaji mkubwa hawa waandishi wa habari wanatumiwa na ccm kupotosha

Habari ilikuwa na upotoshi mkubwa sana kulishwa watu wasio ujua mfumo wa kanda za kichama.
 
Back
Top Bottom