Gazeti la DIMBA uandishi gani huu?

Lucchese DeCavalcante

JF-Expert Member
Jan 10, 2009
5,471
734
Yaani kichwa cha habari chaeleza mchezaji na timu ya ulaya wakati habari yenye ya Bongo tena huku kwetu Mbaaagalaaa, "uandisi" wa bongo bwana...

attachment.php
 
Attachments

  • IMG00930-20100808-1253.jpg
    IMG00930-20100808-1253.jpg
    54.4 KB · Views: 9,274
Kwani African Lyon ni timu ya Ulaya?

Soma kichwa cha habari kinasema Del Pierro ajuta kuitamani Lyon hapo unaposoma kichwa cha habari utategemea kuwa mshambuliaji nguli wa juventus ya Italia Alessandro Del Pierro anatamani kujiunga na Lyon ya Ufaransa lakini kumbe ni habari ya kibongo...
 
Sasa kama timu yetu ya Bongo ina jina hilohilo la Lyon, Mhariri angeiitaje? na huyo kocjha jina lake (la utani) ni hilohilo, sasa Mhariri afanyeje? labda ungependekeza kichwa cha habari kingekuwaje...
 
Waandishi wengine utakuta wanaandika mambo binafsi ya familia ya mtu wanayemzungumzia. Mfano, utakuta mwandishi anaandika: "Akizungumza na gazeti hili, Papic ambaye ni baba wa watoto wawili, Todor na Natasa alisema ...". Sasa hao watoto wanahusianaje na wasomaji wa habari za michezo?
 
Avatar yako nimeipenda sana...
 
Waandishi wengine utakuta wanaandika mambo binafsi ya familia ya mtu wanayemzungumzia. Mfano, utakuta mwandishi anaandika: "Akizungumza na gazeti hili, Papic ambaye ni baba wa watoto wawili, Todor na Natasa alisema ...". Sasa hao watoto wanahusianaje na wasomaji wa habari za michezo?

Duh kakaka bongo bado tuko far to the target..nimecheka sana au kuna siku eti Kocha sijui wa Simba sijui yanga ameacha kufundisha mazoezi ili kwenda airport kumpokea mwanae anaetoka serbia..jamani mie nilidhani kimetokea kitu alipoenda kumpokea au vipi...Kaaaaaaaaaziiii kweli kweli BONGO YETU
 
Haya magazeti yetu hasa ya michezo uandishi wao unakera kwelikweli, sijui hakuna wahariri!
 
Waandishi wengine utakuta wanaandika mambo binafsi ya familia ya mtu wanayemzungumzia. Mfano, utakuta mwandishi anaandika: "Akizungumza na gazeti hili, Papic ambaye ni baba wa watoto wawili, Todor na Natasa alisema ...". Sasa hao watoto wanahusianaje na wasomaji wa habari za michezo?
Ila uandishi huu hata ulaya upo na kwenye blogs nimeuona sanaa
 
Labda mimi mnisaidie wadau, kikifanywa Ulaya lazima nasie wabongo tukifanye? Naamini hapa hoja ni kutaka kujua Mwandishi amefanya "kiprofeshenali" au la na siyo afanye tu eti kwa kuwa Ulaya au kwingineko wanafanya!! -- Je tutafika??!!
 
Kitu muhimu ni kuzingatia maadili ya taalumu husika.Gazeti linaloandika habari zilizofanyiwa utafiti wa kina siku zote litapendwa lkn wababaishaji mmmh
 
Soma kichwa cha habari kinasema Del Pierro ajuta kuitamani Lyon hapo unaposoma kichwa cha habari utategemea kuwa mshambuliaji nguli wa juventus ya Italia Alessandro Del Pierro anatamani kujiunga na Lyon ya Ufaransa lakini kumbe ni habari ya kibongo...

We mgumu kuelewa, hiyo ni aka ya huyo kocha
 
Waandishi wengine utakuta wanaandika mambo binafsi ya familia ya mtu wanayemzungumzia. Mfano, utakuta mwandishi anaandika: "Akizungumza na gazeti hili, Papic ambaye ni baba wa watoto wawili, Todor na Natasa alisema ...". Sasa hao watoto wanahusianaje na wasomaji wa habari za michezo?

Tatizo lako Sinkala fitina mno, wangesema Julio Pereila baba wa watoto mapacha roho ingekuwa kwatu.
 
Last edited by a moderator:
Nasikia Barcelona kuna mchezaji anaitwa Lionel Messi a.k.a "Ramadhani Singano" daah bongo tumeendelea sana. J2 njema
 
mm sijaona kosa la mwandishi
ametumia lugha nzuri kupamba gazeti lake,kwani nyie mlitaka nini wakati tayari mmeelewa content yake?
mbona hata humu wengi post zenu ni tofauti na kinachoandikwa ndani lakini tumewakalia kimya tu,ngoja niishie hapa nisijepewa BAN nyingine
 
Back
Top Bottom