Jeshi la Israel limesema kuwa mmoja wa wanajeshi wake ambaye aliaminika kutekwa na wapiganaji wa kipalestina ameuawa katika eneo la Gaza.
Jeshi la Israel limesema kuwa Hadar Goldin aliuawa wakati wa mashambulizi ya Israel katika eneo la Gaza.
Israel ilikuwa imeishtumu Hamas kwa kumteka mwanajeshi huyo ,ambapo wapiganaji hao walikana madai hayo.
Waziri mkuu nchni Israel Benjamin Netanyahu amesema kuwa Israel itaendeleza oparesheni zake katika eneo la Gaza hadi pale usalama wa raia wa Israel utakapoimarika.
Hamas imesema kuwa itaendelea kupigana hadi pale itakapoafikia lengo lake.
Kundi hilo linataka kuhakikishiwa kuwa Israel na Misri zitafungua kizuizi cha mpakani cha miaka 7 kilichowekwa katka eneo la Gaza.
Hodar Goldin mwanajeshi wa Israel aliyeuawa
CHANZO: BBC

Mwanajeshi wa Israel aliyepotea, ameuwawa
Jeshi la Israel leo(03.08.2014) limetangaza kifo cha Hadar Goldin, mwanajeshi ambaye alipotea katika ukanda wa Gaza siku mbili zilizopita, huku hali ya umwagaji damu ikiendelea bila kuwa na matumaini ya kufikia mwisho.
![]()
Luteni Hadar Goldin aliyeuwawa katika mapambano Gaza
Tume maalum inayoongozwa na mkuu wa masuala ya kidini wa jeshi hilo, rabbi , amesema luteni Goldin ameuwawa katika mapambano katika ukanda wa Gaza siku ya Ijumaa, jeshi la Israel limesema katika taarifa. Msemaji wa jeshi amekataa kusema iwapo mwili wa mwanajeshi huyo umepatikana ama la.
Upande wa Israel hapo kabla ulionesha hisia kuwa mwanajeshi huyo mwenye umri wa miaka 23 Goldin amekamatwa mateka na wapiganaji wa Hamas katika ukanda wa Gaza, na kutoa nafasi finyu ya kuwapo makubaliano ya muda mrefu ya kusitisha mapigano katika mzozo huo uliosababisha umwagikaji mkubwa wa damu.
Uchukuaji mateka unaonekana na Israel kuwa ni kama kuiweka nchi hiyo rehani.
Tawi la kijeshi la Hamas , la Ezzedine al-Qassam, limekiri kuwa wapiganaji wake wamefanya shambulio la kushitukiza mapema siku ya Ijumaa ambapo wanajeshi wawili wa Israel wameuwawa, lakini imekana kumshikilia Goldin.
CHANZO: DW