Gavana Shilatu acharuka

wandamba

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2014
Posts
510
Reaction score
839
Na Mwandishi wetu, Mihambwe

Michezo ya Pool table, sehemu wanazouza vilevi, michezo ya Bonanza na mabanda ya video yamepigwa marufuku kufunguliwa saa za Kazi na Watoto chini ya miaka 18 kukatazwa kabisa kujihusisha nayo ndani ya Tarafa ya Mihambwe.

Hayo yamebainishwa na Afisa Tarafa Mihambwe, Emmanuel Shilatu alipokuwa akipitia kwenye sehemu zenye michezo hiyo na kuagiza mambo hayo yafunguliwe kuanzia saa 10 jioni siku za Kazi na ni marufuku Watoto chini ya miaka 18 kuonekana maeneo hayo.

*"Watu hawafanyi Kazi kutwa kwenye Pool table na baa; Watu wanafilisika kisa Mabonanza; Mabanda ya video yamekuwa vichaka vya Wanafunzi watoro na mmomonyoko wa maadili. Tarafa ya Mihambwe tumedhamiria Watu wafanye Kazi, Wanafunzi wasome na si vinginevyo. Watoto chini ya miaka 18 ni marufuku kabisa maeneo haya na muda wa kufungua ni kuanzia saa 10 jioni siku za Kazi. Hivi karibuni nilikutana na Watendaji Kata nikawapa maagizo washirikiane na Watendaji Vijiji pamoja na Polisi kuhakikisha wanakula sahani moja na wavunjifu wa Sheria, Taratibu na Kanuni za Nchi."* Alisema Gavana Shilatu.

Gavana Shilatu alibainisha lengo la Serikali ndani ya Tarafa ya Mihambwe ni kuhakikisha inalinda maadili na ustawi wa maendeleo ndani ya jamii.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu jamaa anapenda kiki,mambo ya mtaani mpaka ayaweke public.
 
Naona jamaa anajitahidi kujitengenezea kiki labda mkuu atamuona akampa uDC

Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa kiki ni ipi hapo

Hivi tanzania tuna uchumi gani wa mtu kucheza pool table na michezo ya bonanza asubuh mpaka usiku wa manane , by looking at reality ya hao watu wanaocheza plus students

Tuangalie sera za wachina na wajapana mpka kufikia kuwa first class countries au sera ya nchi yeyote ile je waliwekeza katika imastable issues kama hizi !?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwenzie alianza kwa mbweeeembwee mara kaufyata! Kuanzia mwezi wa pili monde 24/7
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…