Garatwa: Tangu nijiunge na CHADEMA sijawahi kuona Upendo mkubwa wa TBC kama huu wanaomwonesha Mwenyekiti wetu Mbowe sasa, Je huyu Mbowe ni huyu huyu?

Kompyuta imeingiliwa na virus na haiwezi kufanya kazi ipasavyo hivyo kinachohitajika ni kupata Antivirus software ili kumpyuta irudi kama mwanzo.
 
Nami naona upungufu mkubwa katika akili yako unayo jivunia hapa.

Ndiyo, ni kweli kabisa kuwa uhai wa chama huko mitaani na kwingineko ni jinsi wananchi, wanachama wenyewe wanavyo jitoa na kuchangia shughuli za chama chao mahali walipo. Hili halina mjadala. Unapo pungukiwa na akili wewe mwenyewe ni kutotambua wajibu wa uongozi wa juu katika kuunga juhudi hizi za wana chama huko waliko wakijishughulisha na ujenzi wa chama chao.
Kwa nini wewe unafikiri hiyo ruzuku haiwahusu wao, wananchi huko mitaani, ili kuongeza nguvu za wananchi wenyewe kufanikisha shughuli za chama chao; na badala yake iwe ni kwa viongozi makao makuu; akina Mbowe kutumia 'chopa' hata kwenye mikutano isiyo kuwa na manufaa yoyote?

Ungeniuliza mimi, nimgekueleza kuwa hiyo ruzuku ingetumika zaidi katika shughuli za chama huko mitaani, vijijini, kwenye kata, kwenye wilaya, n.k., kwa sababu huko ndiko kunako hitajika nguvu kubwa kuwa'mobilise' wananchi; ambao ndio wenye maamuzi ya mwisho katika kila jambo ndani ya nchi hii.

Unalipia chopa mamilioni kwenda kuhutubia watu kijumla jumla tu; wakati pesa hiyo hiyo ingeweza kuzaa matokeo makubwa zaidi inge elekezwa kwa wananchi katika eneo hilo kwa maswala ambayo ni ya kimkakati!

Sasa usije hapa na kusema kuwa sitambui umuhimu wa hiyo mikutano yote ya hizo chopa au njia zinginezo za viongozi kuwafikia wananchi huko waliko kwa mpangilio mahsusi.
 
We tafuna au utapike hatuwezi kumpa chizi chama.
Hebu tueleze lisu amekua mbunge jimboni kwake ni kitu gani wananchi wanaweza wakajivunia lisu kuwaketea.
 
..umeandika kwa sababu najivunia akili? hujui kitu chochote..usidhani uanachama wa saccos ni sawa na ule wa vyama vya siasa..vyama vya siasa vina katiba na majukumu ya kufanya hadi wanachama wa tawi jipya la chama linapofunguliwa, liwe na wanachama wangapi, wanaweza kufanya mambo gani kujenga chama kwenye eneo lao nk nk..na usilinganishe majukumu kwa namna ulivyosema..matumizi ya kampeni za uchaguzi ni tofauti na shughuli za chama za kila siku..
mambo ya kutoa fedha makao makuu kupeleka chini kulipia mambo ambayo wanachama wa eneo husika wanaweza kufanya ndio yamewafikisha ccm hapo walipo, kukisalimisha chama chao kwa matajiri na mercenaries kwa gharama ya kupoteza nguvu ya wanachama kufanya maamuzi..ni upumbavu kupita njia ya kijinga km hiyo!
 
Mbowe ni insulator ya baina ya Upinzani ( chadema) na CCM. Kazi yake ni kubalance harakati za kisiasa.

Huyo siyo mpinzani ni mtumishi wa CCM.
Wewe umeshindwa nini kuwa mpinzani? katiba ya nchi hairuhusu?
 
.umeandika kwa sababu najivunia akili?
Hapana, sijaandika hivyo. Naomba unielewe, ni kinyume chake. Na haya yaliyo fuata ni kielelezo sahihi cha niliyo eleza hapo.
Sasa kama bado unayo mashaka, na huelewi ninacho kueleza hapa, basi hilo ni tatizo kubwa.
 
Lakini pamoja na kuto kubaliana na wewe katika hayo ya kule mwanzo; kwenye haya hapa ninakubaliana na wewe.
CCM ambayo wana chama wake walikuwa wakijenga ofisi siku zile, siyo CCM ya siku hizi.

Msisitzo, ambao pengine hatutofautiani kati yetu ni kwamba chama ni lazima kiwe cha wananchi. Wananchi wajihusishe na shughuli za chama chao kila mahali walipo, na wawe tayari kukipigania chama inapo hitajika.
Lakini haya hayawezi kupatikana bila ya ushiriki/uhusika wa viongozi wakuu na kutolewa kwa misaada mahali ambapo nguvu za wananchi hazijitoshelezi.
Wananchi wakifahamu wajibu wa viongozi wao wa ngazi zote, sioni kwa nini chama kisiimarike huko mitaani, vijijini na kwingineko.
Nirudie, mikutano ya hadhara ya viongozi wakuu siyo ujenzi wa chama. Mikutano hiyo ni uhamasishaji tu baada ya kazi kubwa kufanyika katika ngazi za mwanzo kabisa.
 
Mnalia lia nini? Demokrasia inazunguza nani ataongoza CDM.

Dawa ni sanduku la Kura - Mbowe vs Lissu.
Hakuna opton nyingime kwa sasa.
 
Wapumbavu wa ccm ni wengi, nyie watu akili zenu fupi sana.
 
Kwa upande wa TBC, mbona siku Tundu Lissu alipokutana na waandishi wa habari TBC pia walikuwepo? Hata kama watu Wana mapenzi na Lissu kuwa fair pande zote. Ushabiki wa namna hii bure kabisa!
 
Afadhali umeliumbua hilo linafiki
Hata kwa Tundu Lissu TBC ili'cover' conference yake na waandishi wa habari. Sasa kama TBC ku'cover' conference ya Mbowe anakuwa "linafiki", then TBC ku'cover' conference ya Lissu naye anakuwa "linafiki". Hapo vipi?
 
Dr Nchimbie si.mtu.wa mchezo kaja kaivunja chadema broad day light kwa.strategy kali.sana
Unajitekenya Kisha unacheka! Huo ni ukichaa. Yaani Lissu anagombea uenyekiti kwa maelekezo ya Nchimbi! Huu ujinga mtupu.
 
Hapana, sijaandika hivyo. Naomba unielewe, ni kinyume chake.
Na haya yaliyo fuata ni kielelezo sahihi cha niliyo eleza hapo.
Sasa kama bado unayo mashaka, na huelewi ninacho kueleza hapa, basi hilo ni tatizo kubwa.
..maneno meeengi hadi mwisho umeshasahau yale ya mwanzo..anyway kp your ignorance t s good fr you.
 
Mbowe ni muuaji nikiwaambieni mnafanya dharau maneno yangu
 
TBC ni chombo cha Uma na hivyo kina jukumu la kuonesha matukio yote bila kujali chama.
Hata hivyo, kwa sababu ya fikra za kitumwa ambazo bado zipo miongoni mwa jamii nyingi za kiafrika na Tanzania ikiwemo, watumishi wa vyombo vya dola hujipendekeza kwa chama tawala bila hata kulazimishwa.
Changamoto ni matumizi mabaya ya madaraka kwa baadhi ya viongozi ambao hulazimisha na hata kuwafuta kazi watumishi wanaojielewa (rejea tuhuma zinazohusiana na mkataba wa Tido Mhando) .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…