SautiYaMnyonge
JF-Expert Member
- May 13, 2018
- 439
- 742
Na Mwandishi Wetu
Bomang'ombe, Hai.
Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa (NEC) na Naibu Katibu Mkuu UVCCM Tanzania Bara Ndugu Galila R. Wabanh'u ameshiriki uzinduzi wa ujenzi wa madarasa matatu na maabara ya sayansi katika shule ya sekondari ya Wari inayomilikiwa na umoja wa wazazi Tanzania, Jumuiya ya CCM. Akiwa shuleni hapo Ndugu Galila ameendesha pia zoezi la kuchangia kukamilisha ujenzi huo.
"Wadau wengi katika jamii walivunjika moyo kuchangia fedha katika shughuli za maendeleo kutokana na fedha hizo kutumika kinyume na lengo la kuzichangisha. Hivyo ni vizuri pamoja na kuwa waaminifu katika matumizi ya fedha zinazochangwa kufanikisha ujenzi huu, himizeni michango ya vifaa vya ujenzi (building materials) zaidi kuliko fedha. Hapa kila mtu atatoa na lengo litafikiwa.
Uchangiaji wa shughuli za maendeleo katika jamii haituhitaji tuwe matajiri au wenye uchumi mkubwa bali tunahitajika tu kuwa na moyo wa kujitolea. Hakuna mchango mdogo katika kufanikisha shughuli hizi za maendeleo hivyo ni vyema kila anayeguswa kushiriki kwa chochote tumpe nafasi ashiriki."
Katika kuwa mstari wa mbele kufanikisha ujenzi huu Ndugu Galila aliongoza changizo fupi ambapo yeye binafsi alichangia bati 200 na miavuli 10 kwa ajili ya wanafunzi kujisomea mchana na usiku kwani giza likiingia huwaka taa. Aliungwa mkono na marafiki zake, viongozi wa chama na serikali waliojitokeza kushiriki. Ambapo zilipatikana bati 220, tofali 1,000, mifuko 125 ya saruji, lori 3 za mawe na fedha kiasi cha 2,379,000/-.
Pia Ndugu Galila amechangia jezi kwa ajili ya mazoezi kwa wanafunzi (jogging), timu za mpira wa miguu, mpira wa pete, mipira pamoja na Televisheni moja.
Ndugu Galila alipata nafasi ya kujionea na kukagua ujenzi wa jengo la kinywa na meno ambalo linajengwa kwa gharama ya milioni 84 fedha za mapato ya ndani ya hospital ya Wilaya ya Hai ambapo amewachangia vigae vya sakafuni (tiles) ili kukamilisha ujenzi wake. Vile vile ameiagiza jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Kilimanjaro na wilaya ya Hai kwenda hospitalini hapo na kupanda miti ili kuipa mazingira mazuri.
Katika kumalizia ziara yake Ndugu Galila alifanikiwa kuongea na vijana wa sekondari ya Hai ambapo aliwakabidhi kadi za UVCCM vijana 183, kuwachangia jezi za mpira wa miguu na twlevisheni moja huku mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Hai akilipia king'amuzi watakachokichagua wanafunzi kifurushi cha mwaka mmoja.
Akiongea na vijana hawa aliwahimiza wamechagua chama sahihi kwao kufanya siasa, kujifunza uongozi na kujifunza historia ya nchi yao. Amewataka kuendelea kuiunga mkono CCM na serikali yake hususani kuyasemea mafanikio ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi pamoja na kuwa watetezi wa Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli dhidi ya wapinga maendeleo.
"Tumempata Rais mzalendo kwa vitendo. Aliyeamua maliasili na rasilimali tulizo nazo zinatumika kwa maendeleo yetu. Kazi hii sio nyepesi ni ya kujitoa muhanga kwelikweli. Tumuunge mkono na kumuombea kwa Mungu ili amlinde afanikishe kuipa nchi yetu ukombozi wa pili, ukombozi wa kiuchumi." Alisema Galila
Galila aliendelea kusisitiza kuwa "Rais Magufuli ametambua ni wajibu wetu sisi watanzania kuijenga nchi yetu ndio maana anahimiza nidhamu na uadilifu katika kusimamia rasilimali fedha za umma ili kufikia malengo hasa ukizingatia ni mtu anayependa kuona au Kupata matokeo kwa kile anachokisimamia. Ndio maana vita dhidi ya rushwa na ufisadi ameamua kuipigana jumla jumla na matokeo yanaonekana kwani tumeshuhudia walioiba fedha za umma wakirejesha huku nchi ikifanikisha utekelezaji wa miradi mikubwa ya kiuchumi."
Ndugu Galila aliwataka vijana hao wapya kuwa wazalendo na kupenda kuitangaza nchi yetu kwa mambo chanya. Huku akiwaahidi changamoto nyingine zilizobaki ataziwasilisha katika mamlaka za juu kwa utatuzi hususani uhitaji wa matundu ya vyoo, mabweni na walimu wa masomo ya sayansi kwa wanafunzi wa kidato cha tano na sita.
#TupigeVitaUjinga
#MagufuliChaguoLetu
#MaamuziYetuCCM2020
Sent using Jamii Forums mobile app