PreGE2025 G55 wanapaswa kusimamishwa uanachama CHADEMA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Annunaki

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2021
Posts
2,210
Reaction score
4,631
Bado nitaendelea na msimamo ule ule wa CHADEMA kuwafuta uanachama, wanachama wanaotaka kukwamisha mipango ya chama.

Kama ningekuwa sehemu ya maamuzi ya CHADEMA, ningeshauri wajibiwe hoja zao zote kwa maandishi, na baada ya hapo utaratibu wa kuwasimamisha uanachama uanze mara moja.

CHADEMA haiwezi kutekeleza agenda zake ikiwa itaendelea kuwakumbatia watu wa namna hii.

Vile vile ni hawa hawa G55 baada ya uchaguzi wamekuwa wakileta chokochoko za kukikwamisha chama.

Kama waliweza kuwafuta uanachama covid 19, hawa G55 wana nini cha ziada kwenye chama zaidi ya kukwamisha harakati za chama.

Hapa chini ni baadhi ya hoja zao;
 

Attachments

  • 20250404_180821.jpg
    133.4 KB · Views: 22
Sio kusimamishwa tu ni kuwafukuzia mbali wasaliti hao.Mungu kaamua kuwaonyesha mapema na ubinafsi wao,wanawaza uongozi bila kujali maisha ya watu yanapotea kisa uchaguzi wa hovyo.
 
Jamaa wana calculations kali, watapiga sana pesa ya mama na mwanaye.

Mkubwa na wanaye😅😅
 
Sio kusimamishwa tu ni kuwafukuzia mbali wasaliti hao.Mungu kaamua kuwaonyesha mapema na ubinafsi wao,wanawaza uongozi bila kujali maisha ya watu yanapotea kisa uchaguzi wa hovyo.
Wajinga sana Hawa G55. Kwamba wao hawaoni kinachojiri nyakati za uchaguzi!?
 
Nadhani wanapaswa kuelimishwa tu, Wajibiwe kwa hoja na waonyeshwe Makaburi ya Wanachadema waliouawa kwa sababu za Uchaguzi ambayo yako nchi nzima, ninaamini wataelewa tu, kuwafukuza hakuna sababu wala tija yoyote
 
Bila kuuana hakuna mabadiliko.
 
Unaweza Kuta hiki kikundi Cha wahuni kinaratibiwa na Makalla
 
Unawaacha, ukiwafukuza unawapa umaarufu, unawaacha wapige yowe mpaka sauti ikate, ukiwajibu unawapa kick
 
Sema Makamanda mnatakiwa kuwa makini sana mnapo pambana na hao G55! Kwa sababu wana hoja ya msingi. Na pia kitendo walichokifanya ni cha kidemokrasia! Kwa hiyo wanatakiwa wasikilizwe, badala ya kutishwa.

Yaani kwa CCM mkisusia ndiyo wanapenda ili wakose upinzani wa kweli! Na wakati huo huo mkishiriki, unakuta tayari wameshaandaa mbinu zao ovu za kuiba kura! Huku policcm wakiwekwa tayari kwa ajili ya kuwadhibiti wale wanachama wote wataotaka kuzilinda kura zao! Na tume yenyewe kama ilivyoundwa, ni kiini macho tu!!

Yaani CHADEMA mnatakiwa mje na namna bora ya kupambana na hila za CCM! Zamani walikuwa wanaiba hizo kura kistaarabu! Ila kuanzia 2019, 2020, na 2024; umekuwa siyo wizi tena wa kura! Isipokuwa ni uporaji!

Je, mtakuja na mbinu gani za kuudhibiti huu uporaji mpya wa kura? Kususia, bado haisaidii! Labda muwe na ujasiri wa kukinukisha kudai haki yenu kama walivyofanya wale jamaa wa Msumbiji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…