Fursa za biashara nchi ya Thailand

Safi sana kiongozo kwa kutufungua macho.Ubarikiwe sana.Nitakupm one day tuzungumze vizuri.

Ngoja nidundulize fedha.
 
vitu adimu sana hivi mkuu asante sana kwa moyo wa kipekee ulionao kwasababu wapo wengi wanajua mengi lakini hawataki kuwaelekeza wengine!! Mungu akubariki sana umetufungua na wengine sikuwahi kuiwazia hiyo nchi!!!
 
Safi sana kiongozo kwa kutufungua macho.Ubarikiwe sana.Nitakupm one day tuzungumze vizuri.

Ngoja nidundulize fedha.

Hizo bei alizosema $ stuna ni kweli kabisa..lakini nchi yetu ilivyo si kila mtu anawezafanya biashara hizi za ku IMPORT,mbali ya kusafiri,kununua na kutuma bidhaa kizingiti kikubwa kipo kwenye kodi,kodi zetu hazieleweki kabisa X akinunua bidhaa hii ushuru ni huu na Y akinunua bidhaa ileile ushuru ni tofauti kabisa,nikupe mfano kidogo kuna siku nilifunga container na kulisafirisha Tz,ndani kulikuwa na vitu mchanganyiko kulikuwa na baiskeli moja ya mtoto ambayo nilinunua $30 lakini Tra wali uplift na ktk hesabu zao wakasema ni $120 hivyo ushuru ukaja wa ajabu sana,ndio maana unaona watu wanashindwa kutoa vitu bandarini.Gharama ya kuingiza kijigari kidogo kama Vitz ya 2004 Nigeria ni $1200 Uganda wasio na bandari ni $1570 Tz ni almost $2000 mpaka kuiweka njiani!!!ndio maana leo watu wanatoka Tz kwenye bandari kwenda kununua bidhaa Rwanda/Uganda kusiko na bandari????Bidhaa nje ni rahisi lakini si kila mtu anawezafanya biz ya kuingiza bidhaa nchini.Kuna watu container la ft 20 lenye cement wanatoa ushuru wa 1.8ml maana mfuko mmoja wa cement Dubai ni Tsh 2500/mimi pia nilituma langu jamaa Tra wakanipiga 3.2ml..Wengine wanapitisha bidhaa port lakini wengine wakipitisha bidhaa zilezile basi TBS wanazichoma moto eti ni FAKE
 
kwahiyo tatizo ni TRA...hawa jamaa wanarudisha nyuma sana wafanyabiashara.
 
Kweli hawa Tra wanaturudisha nyuma kweli.
Ila vipi kuhusu bidhaa ambaza hazilipiwi ushuru kama computers, printers etc. Vitasumbua kutoa bandarini?
 
mkuu shukrani kwa kutupatia source ya ujasiliamali ambayo wabongo wengi ni vigumu kuwapatia wenzao
 

Mkuu tunashukuru sana kwa taarifa mhimu sana. Unaonekana wewe ni Mtanzania mzalendo sana. Maana taarifa pekee ni fedha. Watu wanafedha ila hawana taarifa nini cha kufanya. Labda mkuu vipi kuhusu vurugu za waandamanaji zinazoendelea kila kukicha huko thailand si ni tatizo kwa wageni wanaoingia humo?
 

vurugu za maandamano uwa azi affect sana biashara sababu zinafanyika maeneo yenye ofisi za serikali kama wizara ya fedha etc.

maeneo ya biashara na utalii hakuna maandamano. hivo biashara zipo kama kawa. mitaa yenye ofis za serikali ndio uwa kinanuka
 
Mkuu MONEYstuna asante sna kwa taarifa samahani waweza nambia nauli ya go and return pamoja na visa
 
Last edited by a moderator:


Ahsante Mkuu
 
Mkuu MONEYstuna asante sna kwa taarifa samahani waweza nambia nauli ya go and return pamoja na visa

Wasiliana na hizi kampuni za kukatisha ticket watakusaidia taratibu zote adi visa pia wanakatisha ticket za ndani na kimataifa.

Wing Travel Limited
simu : 255 22 2120675
Website www.winglink.net/blog/

Pia Travel start
Simu 255 222124881/2
Website www.travelstart.co.tz

Wasiliana nao wote mwisho wa siku utachagua yupi akusaidie visa na ticket
 
Last edited by a moderator:

Mbona nimeipenda hiyo ya cement je wewe hajaweza kujua mbinu gani wanatumia ili tulipe ushuru kidogo! nahitaji sana cement ndugu!
 
Hizo namba zinaweza kukusaidia pia Bangkok kuna watu wa kila aina sijaona ubaguzi.

Usalama upo

shukran kwa taarifa mkuu,
nimewafahamu kibiashara kama dazeni moja ya wathai ndani ya Tz, wanaonekana kana kwamba maisha yao ya kibiashara si tofauti sana na wachina na wana magenge ya uhalifu wa kibiashashara pia.

Kwa mtu anayepeleka biashara kwao usalama ni wa uhakika?, au pia kuna sehemu za kuepuka?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…