Wasalaam!
Je, una wazo zuri la biashara lakini huna mtaji wa kuanzisha? Hii ni fursa yako.
Nina mtaji wa
TSh Milioni 10 na kutokana na majukumu mengi ya kazi nashindwa kujigawa, ninatafuta
kijana mwenye wazo la biashara lenye tija na uwezo wa kusimamia biashara hiyo kwa uadilifu, uwajibikaji na weledi.
Maeneo ya Biashara
Biashara inapendekezwa kufanyika katika
Mkoa wa Dar es Salaam na Mkoa wa Pwani.
Mahitaji
- Awe na wazo la biashara linalotekelezeka na lenye faida.
- Aandae mpango kazi (Business Plan) unaoelezea:
- Aina ya biashara
- Mahitaji ya mtaji
- Makadirio ya mapato na matumizi
- Mikakati ya ukuaji wa biashara
- Jukumu lake katika usimamizi wa biashara
- Awe tayari kushirikiana kwa uwazi na uwajibikaji.
Jinsi ya Kutuma Maombi
Tuma mpango wako wa biashara pamoja na maelezo mafupi binafsi.kwa njia ya PM
📅
Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 30 Oktoba 2026.
📞
Mwombaji atakayechaguliwa atapigiwa simu tarehe 30 Novemba 2026.
Ni vijana wenye nia ya dhati, ubunifu na uwezo wa kusimamia biashara watakaozingatiwa.
KARIBUNI SANA NA KWA UAMINIFU MKUBWA.