vijana changamkieni fursa hiyo!Wasalaam!
Je, una wazo zuri la biashara lakini huna mtaji wa kuanzisha? Hii ni fursa yako.
Nina mtaji wa TSh Milioni 10 na kutokana na majukumu mengi ya Kigalinashindwa kujigawa, ninatafuta kijana mwenye wazo la biashara lenye tija na uwezo wa kusimamia biashara hiyo kwa uadilifu, uwajibikaji na weledi.
Maeneo ya Biashara
Biashara inapendekezwa kufanyika katika Mkoa wa Dar es Salaam na Mkoa wa Pwani.
Mahitaji
- Awe na wazo la biashara linalotekelezeka na lenye faida.
- Aandae mpango kazi (Business Plan) unaoelezea:
- Aina ya biashara
- Mahitaji ya mtaji
- Makadirio ya mapato na matumizi
- Mikakati ya ukuaji wa biashara
- Jukumu lake katika usimamizi wa biashara
- Awe tayari kushirikiana kwa uwazi na uwajibikaji.
Jinsi ya Kutuma Maombi
Tuma mpango wako wa biashara pamoja na maelezo mafupi binafsi.kwa njia ya PM
π Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 30 Oktoba 2026.
π Mwombaji atakayechaguliwa atapigiwa simu tarehe 30 Novemba 2026.
Ni vijana wenye nia ya dhati, ubunifu na uwezo wa kusimamia biashara watakaozingatiwa.
KARIBUNI SANA NA KWA UAMINIFU MKUBWA.
ok wanakujaHapa ndipo tunaanza kutofautiana Kati ya wapambanani na wabangaizaji.
Risk takers watafanya. Kikubwa nataka mtu anaejua anachokifanya. Asiwe mtu wa kuiga bila kujua mpango kazi.
Kwenye upepoHayo maombo yanatumwa kwa njian ipi?
Tunatuma wapi maombi hakuna hata email
Mshafeli intavyuu bros acheni tu.....Hayo maombo yanatumwa kwa njian ipi?
Kwakweli..πMshafeli intavyuu bros acheni tu.....
Kweli kbsa kumbe alishatoa site ya kutuma maombiπMshafeli intavyuu bros acheni tu.....
Bro usimpangie boss πKwakweli..π
Ila kutuma business plan pm ni jambo la ajabu, mtu aliye serious aweke email!
πππ Hadi hapo chaliiiiiKweli kbsa kumbe alishatoa site ya kutuma maombiπ
ππ€£π€£π€£π€£πππ Hadi hapo chaliiiii
Nimesoma pale alipoandika ana majukumu mengi nikajua huyu anataka business idea kiulainivijana changamkieni fursa hiyo!
Angalizo: msije kuwa nyie ndio fursa yenyewe
Huu ndo msumari wa motoNinq wazo, nina mipango tayari, na nia ya kuliendeleza, issue ni mbili, kwanza mimi si kijana, ni mtu mzima ninayesogelea uzee, pili mimi pia nina issues nyingine zinazoniweka busy muda mwingi, so ni either nikuuzie wazo langu alongside strategies, au tuungane kuli accomplish in other way possible, karibu boss.