Fursa kwa wanachuo na wenye stationary n.k

Fursa kwa wanachuo na wenye stationary n.k

mtengwa

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2011
Posts
1,604
Reaction score
872
habari wadau
kuna fursa napenda ni share na wenzangu ambao wana stationary na wanafunzi wa chuo ambao kwa mtaji mdogo usio zidi laki 1 wanaweza kupata hela ya kujikimu na ugumu wa maisha wakiwa chuoni.


wazo lenyewe ni hili

kama unavyojua mahitaji ya flash disc na memorya cards kwa wanafunzi wa chuo, hivyo basi kwa mtaji mdogo unaweza kununua bidhaa hizo kutoka kwangu na kuziuza kwa bei yenye faida.


Flash Disc na Memory Cards ambazo ni original na zina warranty nauza kwa jumla
4 gb 8500
8 gb 10000
16 gb 18000

hivyo basi unaweza kuanza na kiasi kidogo tu, ukaagiza mzigo nikakukabidhi then ukaendelea kuongeza kadri ya utakapo uza.

Je, utauzaje?

kwa wanachuo ni rahisi tu, kwanza unaanza kutangazia watu wako wa karibu na kuwauzia pia unatengeneza posters ndogo ndogo au flyers unabandika kwenye notes body za chuo, hostels na sehemu mbali mbali around campus ukiweka bei na namba yako ya simu. hapo wateja watakutafuta tu siku hadi siku na kila mteja mmoja anatengeneza wateja wengine.


bei za kuuzia
kwa reseach niliofanya vyuo vya Dar watu ambao wanafanya biashara hii ambao hawana ofisi bei zao ni hivi

4 gb 12000
8 gb 15000
16 gb 25000

sasa wewe unaweza kushuka kidogo na kuja na bei hii
4 gb 11000
8 gb 14000

vile vile unaweza kupanda kutokana na eneo mfano vyuo vya mikoani.
kwa bei hiyo ambayo ni nafuu zaidi ukiwa na matangazo ya kutosha unaweza kuwa na wastani wa kuuza flash 2 kwa siku ambapo unaweza kuingiza 5000 kwa siku, au zaidi ya hapo bila kuadhiri ratiba zako za vipindi darasani.

Unaweza ukaanza na flash kumi tu
5 za 8 gb
4 za 8 gb
alafu ukaangalia biashara inavyoenda.


Pia kutokana na kufanya online business tutakua tunawa direct wateja wetu ambao wako na eneo ulipo wakanunua bidhaa kwako kwa bei uliyopanga wewe.



Kumbuka biashara hii inahitaji matangazo, hata mtu wa stationary unaweza kuweka tangazo la bei kwenye mlango au sehemu visible kwenye ofisi yako ambapo mteja akija ataiona na atavutiwa na bei kwa sababu sehemu nyingi flash disc wanauza kwa bei ya juu sana hivyo akiona tangazo na bei ni rahisi sana kuvutika kununua kuliko kuziweka ofisini hadi mtu aulizie bei ndo ajue.


Ambao mtakua interested mnaweza kunicheki pm, sms au whatsapp 0714883861.

N:B na mimi nimepitia chuo hivyo najua maisha ya chuo na changamoto, na mahitaji kama haya.
 
Mkuu sio wazo baya,lakini biashaa hiyo haiwezi kusimama zaidi ya miezi mitatu.
Maana Flash disc na Memory cards ni vitu ambavyo kwanza wengi wanatoka navyo A Level.
Pili mnunuaji akinunua basi jua atakata miaka,maana mie ninayo nilinunua tangu 2009 hadi leo ipo.
Sasa ni vitu ambavyo demand yake ni ya muda mfupi sana kwa mazingira ya chuo.
Angalua ungesema rim pepa ambazo zinakaa muda mfupi na ni kama chakula,lazima watu watazitumia on daily basis
 
Mkuu sio wazo baya,lakini biashaa hiyo haiwezi kusimama zaidi ya miezi mitatu.
Maana Flash disc na Memory cards ni vitu ambavyo kwanza wengi wanatoka navyo A Level.
Pili mnunuaji akinunua basi jua atakata miaka,maana mie ninayo nilinunua tangu 2009 hadi leo ipo.
Sasa ni vitu ambavyo demand yake ni ya muda mfupi sana kwa mazingira ya chuo.
Angalua ungesema rim pepa ambazo zinakaa muda mfupi na ni kama chakula,lazima watu watazitumia on daily basis

Me nimefanya biashara hiyo udom CHSS, demand ya flash ipo siku hadi siku, college in wanafunzi zaidi ya 3000 + staff, kwa semister nilikua nauza zaidi ya flash 200
 
Back
Top Bottom