Funzo kwa wanandoa

jangala

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2014
Posts
1,583
Reaction score
2,385
Baada ya mafanikio mke na Mume kumiliki nyumba nzuri .. Mama wa mume kahamia Kwa mwanae... Ila Kwa sababu flani mke na mamkwe havikuiva kama kawaida.
Walianza na chuki kidogo ila kila uchao kukawa vinaongezeka pata shika.
Kwa hasira na maudhi ya mamkwe mdada yule kaamua aende kutafuta dawa ili amuuwe mkwewe. Kafika Kwa docta mwanafalsafa.
Mke: docta nataka dawa ili Mkwe wangu afe au aondoke pale mana kawa tishio kwangu.
Doct: sawa hapa umefika ila kabla ya kukupa dawa niambie mambo yote anayokukera na niambie mambo yote anayoyapenda mkweo.
Mke: (kataja mengiii yote ya kifamilia.) Akamwambia na vyakula na vinywaji avipendavyo.. Kahawa, juice ya miwa.. Nk

Docta akamwambia ntakupa sumu ila sumu hii atakufa pole pole sio ghafla ila ina masharti.
Mke: hata ukisema nikapande Kilimanjaro uchi ntaenda mradi tu nisimuone.
Doct: akanunua kopo la kahawa aipendayo. Akampa masharti.." Kuanzia Leo usimchukie ili akifa usijulikane, mfanyie mambo mema hata akinuna we tabasam, atakacho mfanyie mana siku zake zinaesabika."
...akafika home mke akadumisha Upendo Wa ajabu Kwa mkwewe asubui anamuandalie ile kahawa, mchana a naenda kumletea juice ya miwa, na Zawadi.
Mamkwe nae kuona vile bila kujali nae akarudisha moyo Wa Upendo akampenda mkamwana wake kiasi akimuona mwanae anamgomba basi nae anaingilia kati. Mke sasa akawa anampenda kweli mamkwe wake ila hofu ikamjaa kwamba ndo anakaribia kufa. Akarudi haraka Kwa docta mwanafalsafa ili dawa ibadilishwe.
Docta; dawa hiyo haibadiliki na itaendelea endapo utaendelea Nayo.. Sikukupa sumu Bali nilikuelekeza tu kwamba ukimfanyia MTU jambo alipendalo siku zote mawazo mema na nia njema huleta kivuli chema. Anza Leo kumsalimu adui yako na muoneshe kua una Amani nae hasira zitamshuka..

.....the world is like a mirror if you face it with a smile it smile back to you...
 
Dah hilo sio funzo kwa wanandoa peke yao bali ni funzo kwa watu wote!

Nahisi ulikuwepo kwenye misa ya leo iliyoongozwa na mchungaji Hiza kanisa la CCT mlimani!

Kwa wote waliohudhuria misa hiyo wamefaidi kweli kwa somo hilo maana lilikuwa linagusa maisha halisi ya watu wanavyoishi kwa kutaka/kupenda kulipiza visasi na jinsi ya kuyashinda majaribu hayo ya malipizi mabaya kama ulivyogusia kwenye uzi huu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…