Fununu za wizi

Fununu za wizi

Joined
Jul 23, 2015
Posts
48
Reaction score
12
Mgombea Ubunge wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Jimbo la Ubungo, Saed Kubenea, amedai kuwa zaidi ya kadi milioni mbili za kupigia kura zinatengenezwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kwa ajili kuongeza kura za ziada za kukiwezesha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kushinda katika uchaguzi Oktoba 25, mwaka huu.

Kubenea alidai tayari amepata kadi 100 ambazo alidai amepatiwa baadhi ya maafisa wa Tume ambao walimuahidi kumpatia kadi nyingine zaidi.

“NEC wameweka mkakati wa kukisaidia CCM kupata ushidi katika kufanikisha hilo wametengeneza kadi ambazo hazijajazwa taarifa zozote ambazo wanatarajia kuzitumia kwa kuingiza taarifa za watu ambao hawastahili ili wapige kura,” alidai na kuongeza:

“Tunashukuru kuna wasamaria wema ndani ya NEC ambao hawakubaliani na hujuma hizo, wameamua kutuambia na wametuahidi kutupa kadi nyingine zaidi, na huyo aliyenipa hizi 100 aliniambia hata nikitaka kadi hizo 100,000 atanipa.”

Kubenea alisema tayari amekabidhi kadi hizo kwa mwanasheria na kwamba kabla ya kuzikabidhi, aliapishwa kwanza.

“Naomba NEC iache kufanya kazi za CCM, kama itaendelea kufanya hivi itaipeleka nchi kwenye machafuko, tunaomba ifanye kazi kwa uadilifu na ninamuomba Mwenyekiti wa Tume hiyo asiipeleke nchi pabaya, hatutaki kuona watu ambao hawakuandikishwa wanaingizwa kwenye daftari,” alisema.

Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji, Damian Lubuva, alisema hawezi kuzungumzia chochote kwa kuwa hajaziona kadi hizo.

“Kama CHADEMA wamesema kadi hizo ni za kwetu ni vema wangezileta kwetu ili tuone kama kweli ni zetu, kwa kuwa wamezungumza hayo kwenye mkutano na waandishi wa habari na mimi sijaziona kadi hizo siwezi kuzungumza chochote mpaka nidhibitishe,” alisema Jaji Lubuva na kuongeza:

“Hata nikizungumza hapa itaonekana tunabishana Tume na Chadema, wao kama kweli wanazo watuletee tuthibitishe.”

Naye mgombea ubunge wa Chadema Kawe, Halima Mdee, Halima Mdee, aliitaka Tume hiyo kuhakikisha inahakiki taarifa za wananchi katika vituo vya kupigia kura walivyojiandikishia na si katika kata.

Alisema taarifa ambazo amepata ni kwamba baadhi ya ofisi za wakurugenzi wameambiwa na NEC kwamba wananchi wao watahakiki taarifa zao katika ofisi za kata na si katika vituo walivyojiandikishia kama inavyotakiwa kutokana na uchache wa vitabu.

Jaji Lubuva alisema changamoto za uhakiki wa wapiga kura ni suala ambalo linashughulikiwa kwa kushirikiana na wakurugenzi na kwamba watahakikisha kila aliyejiandikisha anahakikiwa.

Chanzo: Nipashe
 
Wameona hawawezi sasa wsnaanza kulialia ili waonewe huruma ....kubenea naye mhuni tu wala hafai kuwa mbunge kwa kuwa mnafiki mkubwa, kanunuliwa na wahuni
 
Nilipo mwangalia Dr. Shein akijinu hoja ya Maalim, moyo uliniumaaaa yaani mpaka baasi. Halafu wanajiona wajanjaaaaa mpaka. Unawezaje kujitapa kuwa unapendwa huku ukijua wazi kuwa hupendwi?? Kwa nini Tz tunakuwa hivi? Kuishi kimagumashi, kuongoza kimagumashi mpaka hata hewa tunaivuta kimagumashi tu. Je, Tutafika?? Mbwenu, turagoba????
 
ccm ni genge LA wezi kama wanavotuibia escrow.... kuiba kura kwao ni jadi
 
Tutaandaa mashtaka kwa ajili ya The Hague kupitia kadi hizo za kura endapo TUME YA UCHAGUZI na CCM watasababisha maafa kwa ajili ya tamaa ya madaraka.

Afrika inaaibishwa na vyama vilivyoko madarakani hasa vyama vikongwe vinakataa kuondolewa madarakani kwa njia ya kawaida (BALLOT BOX) na kulazimisha kukaa madarakani kwa mkono wa chuma kwa kuwatumia polisi wetu matokeo yake ni vita vya wenyewe kwa wenyewe.

CCM iondoke madarakani kwa heshima kama kweli inawapenda watanzania (of which I doubt).
 
Wameona hawawezi sasa wsnaanza kulialia ili waonewe huruma ....kubenea naye mhuni tu wala hafai kuwa mbunge kwa kuwa mnafiki mkubwa, kanunuliwa na wahuni
Mkuu kwani yeye haruhusiwi kusema kile anachofahamu?
 
Ccm ni genge la wanya nganyi wezi wahuni na mazuzu!
 
ccm kazi wanayo mwaka huu. innaimani hata kama magufuli akipita hawato fanya utumbo kama wamzee wakaya.
 
Ni aibu kujifanya msuluhishi wa jirani (nchi) kwenye migogoro yao kumbe were mwenyewe ndio hatari kabisa kwenye hayo unayosuluhisha.
Ni sawa na mchawi kuhubiri Injili
 
Back
Top Bottom