Al Ahly hawatocheza kwa pressure kali mno endapo mechi inayofuata dhidi ya Al Merreikh watashinda. Maana wakishinda hiyo mechi watakuwa na point 10. Hivyo picha kamili ya kundi hili litapatikana kwenye mechi inayofuata ya Simba vs As Vita na Al Merreikh vs Al Ahly. As Vita akitoa sare au kufungwa atakuwa wameaga mashindano. Huku Al Ahly akimfunga Al Merreikh, mechi ya mwisho ya Al Ahly vs Simba itakuwa ni vita ya kumkwepa Mamelodi (kuongoza kundi)