Fuga App Hatimaye Ipo App Store kwa iPhone 🎉📱

Fuga App Hatimaye Ipo App Store kwa iPhone 🎉📱

Brayan_Jk

Senior Member
Joined
Mar 28, 2025
Posts
187
Reaction score
197
Tunaomba mwaka huu uwe na changamoto chache, faida nyingi, na miradi inayokwenda kama ulivyopanga (au angalau karibu 😅).

Tangu mwezi wa 6 mwaka jana, tumekuwa tukipokea swali hili mara kwa mara:
“Mbona Fuga App haipo App Store?”
“Lini Fuga App inakuja kwenye iPhone?”

Kwa hiyo, kuna habari njema, tunapenda kuwajulisha kuwa kwa wale wote wanaotumia iPhone📱

Fuga App sasa ipo rasmi ndani ya App Store.
IMG-20260207-WA0011.jpg


Kwa wasiofahamu bado, Fuga App ni app inayosaidia wafugaji wa kuku:

Kujifunza ufugaji bora wa kuku (hasa kwa wanaoanza)

Kupata ratiba za chakula za kila siku

Kupata ratiba na ukumbusho wa chanjo

Kusimamia shamba la kuku kwa urahisi na kwa mpangilio


kwa hiyo ukiingia App Store:
Search: Fuga Poultry App
Screenshot_20260206-172257.png

Pakua app, uijaribu, na kama unajua mfugaji wa kuku anayependa kutumia iPhone, tafadhali mshirikishe habari hii.

Tunatumaini mwaka huu tutasikia malalamiko machache ya
“nimesahau chanjo” au “bajeti imepotea katikati” 😄

Kila la heri mwaka huu mpya,
na tufuge kisasa, kwa mpangilio, na kwa faida zaidi. 🐔📊
 
Back
Top Bottom