Kakudanganya nani? Hapo ndio wachezaji wanajiona si lolote si chochote, mechi ya kwanza mmefungwa na timu dhaifu inayoshika mkia, leo mpo na Warusi mnapigwa nyingi, halafu Mbeya city wanapakia vumbi kabisa wapige kwenye mshono.
Nimeona kipindi cha kwanza chote live baina ya CSKA VS Simba, kama Simba beki Mohamed Quattara ameendelea vile vile kuonyesha uzembe anapocheza nafasi ya ulinzi, kibaya zaid kapangwa na Onyango, wote hawana akili, nguvu nyingi maarifa kidogo.
Kocha Robertinho ananitia wasiwasi, kiungo Erasto Nyoni hajacheza takriban mechi 15 pale Simba, amekuwa akisugua benchi sana na wakati mwingine tulibashiri anapelekwa kwa mkopo, Leo kaanza kiungo wa chini kwa timu ambayo ukubwa wake kila mtu anaujua.