Naona ile single ya Chadema ni Zitto imeisha makali, sasa hata hii ya Magufuli ni muda tu usiozidi miaka 10. 2025 upinzani utaibuka kwa nguvu hutaamini. Wasira alisema Chadema itakufa 2013, akaja Kinana nae akasema muungano wa UKAWA ndiyo kaburi lao hawawezi kuelewana. Sasa bora hata muungano wa UKAWA kuliko huo muungano wenu wa Tanganyika na Zanzibar ambao sasa unaunganishwa na bunduki tu lakini watu hawana mpango na huo muungano.