Fredrick Sumaye achukuliwa fomu ya kugombea Uenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Pwani

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
Mwenyekiti wa Dar es Salaam Kuu na Mbunge Wa Ukonga Mh. Mwita Waitara akiwaongozi viongozi mbalimbali wa Mikoa ya Kanda ya Pwani kumchukulia Mh. Fedrick Tluway Sumaye Fomu ya Kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Kanda ya Pwani Kupitia Chadema

IMG-20160713-WA0016.jpg


Mh. Waitara aliongozana na Mwenyekiti wa Mkoa wa Pwani Kamanda Baraka Mwago, Mwenyekiti wa Mkoa wa Ilala Makongoro Mahanga pamoja na viongozi mbalimbali wa Wilaya.na.Majimbo ya Kanda ya Pwani.

IMG-20160713-WA0014.jpg


IMG-20160713-WA0015.jpg


IMG-20160713-WA0013.jpg


IMG-20160713-WA0018.jpg
 
Huyu Mzee kwenye maonyesho ya sabasaba alipohojiwa na Kibonde alionekana kusifia juhudi zinazofanywa na Raisi JPM. Yaani CHADEMA ameenda kimwili tu.
 
hii nchi inahitaji maombi. uhuru tumepata 1961 lakini bado tunakalia siasa za kiukombozi tu badala ya kujenga taifa.
Baada tuwaze jinsi ya kuleta mapinduzi ya kuliko na viwanda tunawaza kukombolewa na sumaye
 
Hii ni udhalilishaji wa ofisi ya waziri mkuu mstaafu.Waziri mkuu mstaafu kugeuka kuwa mwenyekiti wa chama Mkoa?? Hata ingekuwa ni ndani ya CCM it is too low.

Nadhani lengo lake aingie kamati kuu ya CHADEMA.Kaona mwenzie Lowasa kaingia bure yeye kaachwa pembeni ameona apitie dirishani kuingia chumba cha mkutano wa kamati kuu ya CHADEMA kupitia uenyekiti wa CHADEMA mkoa!!

Lakini pia nadhani ni mkakati wa TEAMLOWASA kushika CHADEMA na kuwapiga mateke nje TeamSlaa na TeamMbowe OUT

Vijana wa BAVICHA endeleeni kusota mababu wamekuja kuchukua chama nyie mlie tu
 
Back
Top Bottom