Foundation Course ya Open University

Sadoseba

JF-Expert Member
Feb 17, 2013
243
91
Heshima kwenu wanajamvi.
Naomba yeyote mwenye uelewa kuhusu Foundation Course ya OUT anisaidie maswali yafuatayo:
1. Je, mhitimu aliyefaulu anaweza kuapply University moja kwa moja kupata degree?
2. Ikiwa anaweza kuapply, lazima iwe OUT pekee, au chuo kikuu chochote kile?
Naomba kuwasilisha & naamini mtanisaidia.
 
Asanteni sana kwa michango mizuri.
I wish ningepata na contacts za yeyote aliyepitia Foundation Course, au mwenye full knowledge about it.
Yeyote mwenye real answers naomba apost something plz!
 
Zamani kabla ya TCU kuingia cheti cha Foundation course ungeweza kuingia nacho chuo chochote lakini walipokuja hao TCU wakawa hicho cheti wamefanya ni cheti cha ndani ya chuo!! Kwamba kitatumika ndani ya OUT tu huwezi kwenda nacho chuo kingine kukitumia ingawa kuna watu sijui wanafanyaje utakuta wanasoma Foundation ya OUT then Degree utawakuta wanasoma vyuo vingine kwa kupitia sifa zile za cheti cha Foundation!!

Unaposoma cheti cha Foundation, utasoma masomo matano ambapo mawili ambayo ni ya lazima ni Communication Skills na Development Studies then utakuwa na masomo mengine matatu kutegemea na Bachelor utayotaka kusoma yaan kama unataka kusoma LLB kuna masomo yake, Science pia, Business Administration nayo na hali kadhalika kozi za Faculty ya Arts. Note: Hapa ndipo unatakiwa kuwa makini coz huwezi kusoma Foundation ya Arts then ukataka usome Bachelor ya Science au Business Administration. Upo??

Ni kozi ya almost mwaka mmoja na utatakiwa upate wastani usiopungua 50 ili kuweza kufaulu kuingia Degree!! Yaan alama za Test (/30)zitajumlishwa na Annual (/70)then zitajumlishwa na kugawanywa kwa tano (5) na jibu litalotoka litatakiwa lisiwe chini ya 50 au B.

Ukimaliza na kufaulu kwa wastani huo wa B, utatakiwa kufanya application kuingia Degree sasa. Hii ni ili kuhakikisha kuwa kila hatua unafuatiliwa taarifa zako kwa ukaribu mkubwa.

Naamini kiu yako imekatika ipasavyo sasa?
 
Kuna Dada mmoja kamaliza dip ana GPA ya 2.0 vipi apo anaweza soma faundation ili aende bachelor??
 
Back
Top Bottom