- Saloon za kike na kiume
- vibanda chips
zile sehemu wanazozipenda kufanyia biashara manispaa wangeziboresha na kuwapa namba za kufanyia biashara na zinalipiwa kwa siku au wiki au mweziSource nyingine ni kwa wale wafanya biashara ndogo ndogo ambao wanapanga vitu kwenye bara bara,hao watu na wenyewe ni muhimu kulipa kodi.
hivi wewe ni mwana siasa vile?huna hojaNaona kuna wigo mpana umesahaulika...hebu tujikumbushe
Kodi kwa minara ya simu na yamatangazo ya redio na Televisheni,hakika hili ni eneo jingine ambalo mapato yake yanapotea na ukizingatia ni nyezo zinazoyaingizia makampuni mengi kipato kikubwa na pia wamiliki wa maeneo ya ilipojengwa wanapata mapato mazuri tu tax free.mfano mnara wa simu unaweza kuwa na mita ya kusoma talktime na message zilzotiririka na kutoa wastani wa matumizi iwapo wazo la flat rate lisipokubaliwa
Kodi kwa nyumba za kupanga.Hili ni eneo ambalo limebaki likinufaisha wamiliki wa nyumba bila serikali kupata mapato.naona TRA inatilia mkazo pango la kibiashara lakini haya mapango ya nyumba za kuishi kunapotea mabillion mengi hebu pafanyiwe kazi fasta.majuzi tumesikia TRA wakanzisha mfumo kwa wafanyabiashara wa kipato cha 40,000 kwa mwezi sasa hapo wenye nyumba za kupanga wanawaweka wapi? Maana maapartment yanapangishwa kwa bei za ajabu tena dola mbona wapangaji hawapewi risiti na hao wapangishaji hawana leseni za biashara??
Guest house zilizotapakaa kila kona za miji yetu hazitowi EFD receipt--kuna mapungufu hapo
Bar na groceries everywhere mbona tukiagiza hizo redbull hatupewi EFD?
Daladala tiketi zao pia zingekuwa katika mfumo wa EFD
vilabu vya mpira makato ya viingilio na tiketi ziwe kwa mfumo wa kodi papo hapo
Kumbi za STAREHE NA HARUSI hizi ziwe na kodi per function
na nyinginezo wadau tukumbushane.....
NB; Nimetaja EFD sehemu nyingi lakini ningeshauri mfumo wa EFD uzingatie CREdit SALES kwani ni moja ya huduma inayofanyika na pia pamoja na kuongeza mapato mianya ya matumizi mabaya izibwe kwa kuanzia na wafanyakazi wenyewe wa idara ya Kodi
Nawakilisha mjadala
ndio mimi muuza chips!wewe TRAChangia hoja.. Kama wewe hujaiona wapo wenye akili ndefu wanaiona
tukuweke kundi lipi ama nawe ni muuza chipsi?
Waanze wanasiasa na viongozi wa ngazi za juu serikalini kukatwa kodi kwenye mishahara yao minono.
Misterdennis umenena yaani kwenye exemptions kunatumiaka vibaya watu wanaenjoy tax holiday muda ukiisha wanabadili jina wanaanza upya....!!Rais na wabubunge waanze ili wawe mfano kwa raia wengine.
Income tax act ibadilishwe, zile exemptions zilizoko second schedule ikianzia na mishahara ya marais na kiiinua mgongo cha wabunge!
Source nyingine ni kwa wale wafanya biashara ndogo ndogo ambao wanapanga vitu kwenye bara bara,hao watu na wenyewe ni muhimu kulipa kodi.
Yaani mabaa na hotel nyingi kuna ukwepaji sana na ukidai risiti unaonekana wewe ndo tatizoKwenye mabaa baadhi efd zipo ila hawatoi receipt yaani kama watu wangetoa efd receipt nadhani TRA wangekusanya kodi nyingi sana na wala tusingetegemea wahisani
... Income Tax kwenye magari ya Serikali yanayotumika kwa shughuli binafsi za nyumba, hasa baada ya saa za kazi.
: kwa mfano usiku unakuta STK limepaki kwenye Bar na kumbi za Starehe, watumiaji wanatakiwa kulipa Income Tax.
hawakusanyi vizuri na hawatumii vizuri sasa bora wakusanye zaidi kwa wigo mpana na sio zaidi kwa wigo finyuunataka life lizidi kuwa tight nn? hicho kidogo wanachokusanya TRA wakikikusanya vizuri na serikali ikizuia matumizi mabaya ya fedha na ufisadi inatosha.