kindergarten
Member
- Feb 6, 2017
- 22
- 6
Hii opposion-political masscre inayotekelezwa kwa kunyima watu dhamana inaweza lighalimu taifa. Kunaundwa drama zisizokuwa na major dramatic question ambapo sasa inakuwa zoazoa. Wameona rangi moja hainogeshi wala kung'alisha ukumbi sasa wamechanganya kuwahadaa watanzania. Hii ni ishara ya udhaifu mkubwa sana wa kiutawala ambao hauna dira wala mipango ya kuleta maendeleo kwa njia shilikishi. Ni shangazo kubwa kuona kwamba wale wenye uwezo wa kumudu gharama za mawakili wanakandamizwa. Iweje kachyekwolela mwenzangu. Uongozi si ubabe. Ukiona mtu anakuwa mkali ujue hana mbinu wala maarifa yakinifu kutatua matatizo ya watu. Sasa drama hizi zikiisha wataelekea wapi na kuelekeza makombola wapi. Watazoeleka na ku-perish kama midundo ya bongo fleva inavyo bambata na kubambatuka.