Mimi huwa naamini kila siku kuwa trafiki(askari wa barabarani),ndio husababisha foleni.Yaani hawako fair kabisa;na ukitaka kugundua kuwa hawa jamaa wanasababisha foleni,bahatisha siku na mida hiyohiyo ya foleni upite wakati magari yanaongozwa na taa,yaani foleni zinatembea fasta.
Ushauri wangu:Waziache taa ziongoze magari na wao wawe pembeni tu ku-monitor madereva wanaovunja sheria za barabarani.Na ikitokea taa hazifanyi kazi basi wao ndio wasimame kuongoza magari.Na jambo lingine wazirekebishe hizo taa japo ziruhusu magari kwa muda wa japo dakika 5 au 7 kwa kila upande.