Chukwu emeka
JF-Expert Member
- Jan 12, 2018
- 25,203
- 40,641
Habari wanaJF,
Kuna foleni isiyokuwa na ulazima kwenye eneo hilo,sababu kubwa ni Bandari kavu iliyowekwa siku za karibuni,iitwayo BRAVO, hawa BRAVO hawana eneo la kuegesha malori yao (PARKING) na hivyo wanapark malori yao Barabarani katika eneo ambalo linataa pia na kusababisha foleni bila sababu.
Nchi yetu hii unajiuliza hawa Manispaa ya Ubungo wakipita hapo hawaoni? Kwasababu pamoja na kuleta kero ya foleni,yale malori yanaharibu Barabara,TANROADS inamaana hawaoni na ofisi zao zipo karibu kabisa pale GEREJI.Au ndiyo mpaka Kiongozi apite Wananchi walalamike,na amri itolewe.Kwanini nchi yetu inaendeshwa kiholelaholela tu,kila sehemu mtu anaweza kufanya lolote,au ndiyo RUSHWA watu hawajali.
Kuweka Bandari kavu pale si jambo baya lakini kuifanya Barabara eneo la kuegesha Malori si sawa,ni kero kwa usafiri wa umma na binafsi,watu wanachelewa maeneo ya kazi bila sababu,na jioni watu wanachelewa kurudi majumbani.
Nchi yetu mambo mengi ukiyaona yanachosha sana,tunahitaji reforms kubwa sana maana kila eneo limeoza.
Mfungo mwema 🙏