Fofauti ya Pesa, fedha na Hela ni ipi?

Fofauti ya Pesa, fedha na Hela ni ipi?

Naomba kujua tofauti ya Pesa, fedha na Hela.

Pesa inaweza kukufanya uweze kumudu Kununua tu ama Dagaa na Mnafu kwa sana na Kukopa kwa sana hadi Unaboa huku Usafiri wako mkubwa ukiwa ni wa DalaDala pekee na utaishia Kuishi Nyumba za Kupanga hadi Kifo chako.

Hela inaweza kukufanya uweze kumudu Kununua Utumbo, Nyama kwa kubahatisha, Kukodi Bajaji na Maharage kwa wingi huku ukiwa Unahonga na Moyoni unaumia na ukinunua Magari Mitumba au Mabovu Mabovu.

Fedha inaweza kukufanya uweze kumudu kula Kuku, Nyama, Kumiliki Kampuni yako Binafsi, Kupanda Ndege kwa sana, Kumiliki Magari mapya kabisa na Honga yako ni ya Nyumba au Uwanja.
 
Pesa inaweza kukufanya uweze kumudu Kununua tu ama Dagaa na Mnafu kwa sana na Kukopa kwa sana hadi Unaboa huku Usafiri wako mkubwa ukiwa ni wa DalaDala pekee na utaishia Kuishi Nyumba za Kupanga hadi Kifo chako.

Hela inaweza kukufanya uweze kumudu Kununua Utumbo, Nyama kwa kubahatisha, Kukodi Bajaji na Maharage kwa wingi huku ukiwa Unahonga na Moyoni unaumia na ukinunua Magari Mitumba au Mabovu Mabovu.

Fedha inaweza kukufanya uweze kumudu kula Kuku, Nyama, Kumiliki Kampuni yako Binafsi, Kupanda Ndege kwa sana, Kumiliki Magari mapya kabisa na Honga yako ni ya Nyumba au Uwanja.
Exactly.
Ndiyo maana utasikia ana vipesa au vihela. Hakuna vifedha.
 
...Hapo umrtaja nicknames za fedha. Ni sawa na codrai, cardeti, jeans, lkn zote ni suruali.
 
Exactly.
Ndiyo maana utasikia ana vipesa au vihela. Hakuna vifedha.

Kweli kabisa Kiongozi. Je Wewe hapo upo Kundi lipi? Mimi wala nisifiche nipo katika Kundi ambalo hapo halipo kabila la Kijipesa / Tupesa kwani kwa Shida nilizonazo na Umasikini ulionikithiri huku hali yangu ya Kimaisha Mwenyezi Mungu pekee ndiyo anaijua sina hata huo Uwezo wa Kumiliki hizo Pesa achilia mbali sijui huko kwenye Hela na Fedha.
 
Ukijua tofauti ya Binti,Msichana na Demu utakuwa umefanikiwa pia kujua tofauti ya Pesa, Fedha na Hela.
 
Hela ni vijisenti vinakaa mfukoni kwa ajili ya liquidity, FEDHA zinakaa benki na hazitumiki bila mipango. Pesa ni utohozi tu wa lugha ya Kihispaniola...peso ambayo ni sarafu yao.
 
Yote yana maana moja, ni aina au njia halali za kibali cha kuuza na/au kuna bidhaa. Maneno hayo yametokana na kwamba sisi kama watanzania tumewahi kutumia sarafu hizo kwa vipindi tofauti katika historia:
*1. Fedha:* wakati wa utawala wa kiarabu ambapo fedha(silver) ndio ilikuwa standard currency ambapo zilitofautiana kwa uzito. Yaani mwenye silver nyingi ndio tajiri. Hii ni kama katika nchi za Mashariki ya mbali, Ulaya na Marekani walivyokuwa wanatumia gold

*2. Hela:* hili limetokana na utawala wa kijerumani ambao walikuwa wanatumia sarafu yao iliyoitwa Heller

*3. Pesa:* hii ilikuwa ni sarafu ya Spain, Portugal (Ureno) na Dutch. Iliitwa Pesos

*4. Shilling:* Hii ililetwa na Waingereza katika makoloni yake ambapo kama ambavyo 0.01 ya dollar ya Marekani inaitwa penny na hii shilingi ilikuwa ni kwa ajili ya kutumika kwenye makoloni, yaani £0.05 ilikuwa ndiyo one shilling. Baadaye wakaigawa hiyo sarafu mpya katika vipande 100( kila kimoja kikiitwa cent)

Hitimisho:
Kwa hiyo kuisikia hayo maneno ni kwamba tumeamua kuyatohoa na kuazima ili yatumike katika lugha yetu ila namna yanayotumika kwa sasa ni kutokana kubadilika kwa matumizi ya ile dhana mwanzoni kama nilivyoeleza hapo juu. Ahsante
 
Pesa ni neno lililotoholewa kutoka Spanish (Peso), Hella ni German word na Fedha ni Arabic
Asili ya neno "pesa" katika lugha yaKiswahili ni sarufi ndogo ya Kihindi iliyokuwa kitengo cha rupia. Rupia 1 ilikuwa na "paisa" 64 ikawa sarufi ya kawaida katika Afrika ya Mashariki kabla ya kipindi cha ukoloni. Neno la kiasili "paisa" likanyoshwa kuwa "pesa".

Wajerumani walipoanzisha koloni la Afrika ya Mashariki ya Kijerumani waliendelea kutoa sarafu kwa jina la rupia na pesa hadi 1904. Pesa 64 zilifanya rupie 1. Mwaka 1904 walibadilisha muundo na sarafu ya pesa ilipotea, badala yake heller ilianzishwa. Lakini neno lilibaki katika lugha ikaitwa hela.

Sarafi za pesa zilitolewa na Kampuni ya Kijerumani kwa Afrika ya Mashariki. Zilikuwa na maandishi ya Kiarabu upande mmoja na maandishi ya Kijerumani nyuma yake. Upande wa Kiarabu ulionyesha mawaka wa kutolewa kama tarehe baada ya hijra na upande wa Kijerumani ulionyesha mwaka BK. Maandishi yalikuwa jina la kampuni tu kwa Kiarabu na Kijerumani; upande wa Kijerumani ulikuwa na tai mwenye taji kama nembo laMilki ya Ujerumani.
 
Back
Top Bottom