Fm Academia ndiyo band bora kabisa ya muziki wa dansi

Taborian

Senior Member
Jan 1, 2018
192
222
Binafsi ni mpenzi sana wa muziki wa dansi. Iwe ni dansi ya Tanzania au nje ya Tanzania. Muziki wa dansi asili yake ni Kongo. Hii inahusisha rhumba(dansi ya taratibu) na pia soukous(au sebene ikiitwa Chemko).

Tanzania kuna bendi kadhaa kama msondo, sikinde, diamond sound, twanga na fm academia. Lakini kwangu mimi Fm Academia ndiyo band bora kabisa ya muziki wa dansi. Hizi ni sababu zangu.

1. WATUNZI BORA.
Muziki wa dansi silaha yake kuu mojawapo ni Utunzi wa nyimbo. Fm academia ni bendi yenye tungo zenye watunzi bora sana. Tungo hizi zinagusa nafasi mbalimbali za maisha ya mwanadant. Mf KUHESHIMIANA WANADAMU(Vuta nikuvute, Binadamu), NAFASI YA MWANAMKE(Heshima kwa wanawake, moise katumbi). MAPENZI(Anna, jasmine), UVUMILIVU KATIKA NDOA(Sintosahau).

2. UPIGAJI VYOMBO BORA.
Soukous/sebene inahitaji wapiga vyombo bora sana. Hapa fm academia inao wapiga vyombo bora sana. Mf mpiga guitar la solo Elombe kichinja katika Album ya Vuta nkuvute. Hakika solo limecharazwa ipasavyo.

3. RAPU ZA UBORA WA JUU KABISA.
Hiki ni kionjo cha juu kabisa katika muziki wa dansi. Fm academia wako bora sana katika eneo hili. 'utamu wa vanila eeh utamu'... 'najiuliza hili swali eeh, muzungu na muafrika nani mchawi eeh, mzungu anapaa kwa ndege muafrika anapaa kwa ungo'.

Hizi pia ni baadhi ya sababu kwanini fm academia itasurvive hata bila ya Nyoshi.

Nawasilisha.
 
Nitaanza kuwaheshimu na kuwapenda FM Academia pale tu wakiacha ' Kukopi ' kila kitu kuanzia Nyimbo hadi Uchezaji wao kutoka kwa Bendi za Quarter Latin ya Koffi Olomide na Wenge Musica BCBG ya JB Mpiana. Wanachokifanya tu kubadili tu maneno ya Kilingala, Kiluba na Kifaransa kuwa kwa Kiswahili.
 
sampling sio kosa katika sanaa. Lakini katika nyimbo zao ni kiasi gani wamesample?
 
sampling sio kosa katika sanaa. Lakini katika nyimbo zao ni kiasi gani wamesample?

Utanidanganya kote ila siyo kwa miziki ya Dansi ambayo naijua Kindakindaki na nimeanza kuifuatili tokea nikiwa darasa la tatu way back in late 80's. Hakuna Album ya FM Academia waliotoa hawajaikopi kama ilivyo kutoka kwa ama Quarter Latin au Wenge Musica BCBG.
 
hahaha. Yawezekana u almost 10 yrs older than me, but hujanijibu nilichokieleza mkuu. Nithibitishie ni kiasi gan ngwasuma wamecopy quarter latin na bcbg.
 
hahaha. Yawezekana u almost 10 yrs older than me, but hujanijibu nilichokieleza mkuu. Nithibitishie ni kiasi gan ngwasuma wamecopy quarter latin na bcbg.

Mkuu Wewe ni Nyoosh El Saadat nini mbona unapenda ligi / ubishi hivi?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom