mkuu, sikitika kwanza kabla ya kumlaumu huyu bwana!
Mjasiliamali mzuri daima ni yule anayeweza kubaini gap kati ya kinachotakiwa na wanaokitaka na akitumia hiyo nafasi vizuri ananeemaka.
Shigongo alibaini ujinga wa ndugu zetu wengi kuwa wameathirika na mfumo mbovu wa elimu yetu na badala ya kutumia hiyo nafasi kuwasaidia akaamua kuitumia kwa kuwajaza ujinga zaidi. Na kinachotokea/kitakachotokea huko mbeleni ni ujinga kuongezeka kutokana na 'sumu' aliyotulisha.
Juzi Chameleon alipiga kambi ubalozi wa Tanzania nchini Uganda pale Kagera Road na hilo tukio lili-draw attention ya Waganda na uwezi jua ni wangapi wamejenga mtazamo hasi kuanzia hapo. Yote hayo sababu ya mtu mmoja kufanya mambo ya kipuuzi kwa makusudi mazima.
Ngoja tusubiri lakini historia inaweza kumkumbuka kwa kutumia 'ujinga' wa Watanzania kujitajirisha kama wanasiasa wengine badala ya kutoa mchango wa kuwaelimisha kwa kuwapa ufahamu