Fisi waua kondoo 21 Simiyu

Fisi waua kondoo 21 Simiyu

Mwanantogakulya

Senior Member
Joined
Mar 18, 2025
Posts
130
Reaction score
118
Fisi wameua kondoo 21 huku wengine tisa hawajulikani walipo tukio ambalo limetokea mtaa wa Mahina katika Kata ya Somanda mjini Bariadi mkoani Simiyu.

Mageni Maduhu amesema kuwa tukio hilo limetokea jana April 1,2025 nyumbani kwake majira ya saa 5:00 usiku.

Anasema kuwa alisikia sauti za kundi la fisi wakilia nje ya nyumba yake na alipoamua kutoka nje na kuwakuta na walipomuaona wakakimbia na akaanza kuwakimbiza wakatokomea gizani.

Anasema kwa kuwa yeye ni mfugaji wa kondoo ilimlazimu kuingia katika zizi la kondoo ndipo alipogundua ya kuwa kondoo hao wamekufa huku wengine tisa hawajulikani hawapo hadi sasa.

Matukio ya fisi kuvamia makazi ya watu katika mkoa wa Simiyu yamekuwa yakiripotiwa ambayo yalisababisha vifo kwa watoto tisa katika wilaya za Maswa na Itilima huku zikiwepo taarifa kuwa wapo wananchi wanaomiliki fisi majumbani mwao.
 
Back
Top Bottom