Final count down: 2010 hatudanganyiki!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Final count down: 2010 hatudanganyiki!!!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Nchi Kavu, Oct 26, 2010.

 1. Nchi Kavu

  Nchi Kavu JF-Expert Member

  #1
  Oct 26, 2010
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 3,520
  Likes Received: 1,041
  Trophy Points: 280
  Enyi wana wa nchi
  Nchi yenu i uchi
  Mabedui wanaisachi
  Toka enzi i bichi

  Wameishika pabaya
  Waichezea ka' malaya
  Mwasikia enyi wa kaya
  Chonde muyaelewe haya

  Ndipo ikaja sauti
  Thamani yake Yakuti
  mwanamapinduzi wa dhati
  Wote tumpigie saluti

  Sauti ya jasiri jukwaani
  Inatufuata vyumbani
  Inatusonga mtimani
  :violin:
  Inawatesa kwa yakini

  Mengi yake tumeyasikia
  Pande zote Tanzania
  Anayo dhati na nia
  Kwa jinsi alivyojifunua

  Wa Mtwara hadi Musoma
  Kigoma hadi Mchambawima
  Hima hima hima hima!
  Tuungane Tanzania nzima

  Kikosi kamili kazini
  Chama cha watu makini
  Hakika tupo vitani
  Nchi kuidizaini

  2010 hatudanganyiki!
  Si kwa bia si kaniki
  Twasema dhulma kafariki
  Naisikia harufu ya haki
  2010 HA-TU-DA-NGA-NYI-KI
  :cheer2: :peace:
   
Loading...