Yoyo Zhou
Senior Member
- Jun 16, 2020
- 169
- 287
Takwimu zinaonesha kuwa katika siku ya ufunguzi, jumla ya wanunuzi 64,530 wa ng'ambo wameshiriki katika maonesho hayo, ambalo ni ongezeko la asilimia 8.9 ikilinganishwa na siku kama hiyo mwaka jana, na kuweka rekodi mpya katika historia ya maonesho hayo.
Kama “Maonyesho Namba Moja nchini China”, Maonyesho ya Canton yanachukuliwa kama kiashiria cha biashara ya nje ya China.
Maonyesho hayo ya mwaka huu yamefunguliwa wakati mvutano wa biashara kati ya China na Marekani unapamba moto.
Tarehe 15 Aprili, siku ambayo Maonyesho ya Canton yalifunguliwa, tovuti ya Ikulu ya Marekani ilionesha kuwa China sasa inakabiliwa na ushuru mkubwa kati ya asilimia 125 hadi 245 kwa bidhaa zake zinazoingia Marekani.
Hata hivyo Maonyesho ya 137 ya Canton hayajaathiriwa hata kidogo, na tangu kufunguliwa kwake, yamewashirikisha karibu wanunuzi 150,000 kutoka nchi 216 duniani.
Katika miaka ya hivi karibuni, mawazo ya kupinga utandawazi na vitendo vya kujilinda kibiashara yameongezeka, hali ambayo inatishia ushirikiano wa kimataifa wa kiuchumi na kibiashara. Wakati Marekani “inajenga ukuta wa kibiashara” na “kutenganisha mnyororo wa ugavi”, China inafungua mlango wake zaidi kwa dunia, na wakati inapofanya vizuri mambo ya ndani, inatoa fursa kubwa kwa nyingine duniani.
Maonesho ya mwaka huu ya Canton yanaendelea na mtazamo wa “kufungua mlango na kupata mafanikio ya pamoja”,yameandaa jumla ya vibanda takriban 74,000 katika eneo la mita milioni 1.55 za mraba, na kushirikisha waonyeshaji wapatao 31,000.
Waonyeshaji, wanunuzi na wateja kutoka nchi mbalimbali wametoa “kura ya imani” kwa bidhaa za China, na kuthibitisha kwamba “fimbo ya ushuru” haiwezi kuvunja mnyororo wa biashara ya nje ya China.
Bw. Robert ni mkurugenzi mkuu wa usimamizi wa ununuzi wa ofisi ya Kampuni ya Harbour Freight's ya Marekani mjini Shanghai, China. Kampuni hiyo ina maduka zaidi ya 1,600 nchini Marekani, na anasema asilimia 80 ya bidhaa zake zinatoka China.
Robert amesema, ushuru mkubwa wa Marekani hatimaye utasababisha hasara kwa pande zote. Ameongeza kuwa Kampuni ya Harbour Freight's ina historia ya miaka 30 ya ushirikiano na China, akisema wamekua pamoja na wasambazaji wa China kwa muda mrefu. Kwa hiyo, anatumai kuendelea na ushirikiano huo mzuri na wenzao wa China.
Mfanyabiashara wa Rwanda Said Sultan amesaini mkataba wenye thamani ya zaidi ya dola milioni moja na makampuni ya China kwenye maonesho hayo.
Amesema mnyororo wa ugavi wa China ni muhimu zaidi kwake, kwani bidhaa za China zina ubora mkubwa na bei nafuu, na kukaribishwa sana na wateja wa Afrika.