fikra za utotoni

Socw

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2016
Posts
1,385
Reaction score
2,851
najua wakati tukiwa wadogo tulikuwa na fikra mbalimbali ambazo tulipokua tukagundua kua si kweli..hebu tutiririke hapa...tukianza na mimi
1 nikuwa naamini kuwa dunia imesikiliwa na kakamba kembamba kama utando wa buibui na siku kikikatika ndo kwisha habari yetu
2 nilikuwa naamini kuwa jua hazaliwa asubuhi na linakufa jioni na asubuhi inayofata linazaliwa jingine
3 mvua ikinyesha ni mungu ametema mate
4 radi ikimulika, mungu anatupiga picha
5 ukiweka sindano juu ya reli treni inapata ajali

hebu tiririkeni na nyinyi
 
Ila kwa mtazamo mwingine hizo nyingi ziko sahihi
 
Dah hiyo ya tano ilikuwa tishio sana enzi zangu tena kipindi hicho hata ukimuuliza mtu mzima anakutahadharisha
 
1.Niliamini Mama yangu ndiye aliyemzaa Baba yangu, kwa sababu Tuliambiwa ''mwite Mama/Mama yupo wapi?''

2.Niliamini kuwa mtu kuota ndevu ni matokeo ya kuvuta sigara, kwa sababu hivyo vitu niliviona kwa wanaume tu.

3.Niliamini elimu ya sekondari inaishia form seven, kwa sababu ya msingi mwisho ni STD seven.

4.Niliamini mtu ana uwezo wa kula chakula na kikajaa kwanzia tumboni hadi mdomoni.

5.Niliamini lile anga la bluu ndiye Mungu kwa sababu lipo juu, kila mahali, na nilikubwa, kama nilivyoelezwa sifa za Mungu.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…