Fikra mpya ndio njia sahihi

Fikra mpya ndio njia sahihi

Noor Hassan

Member
Joined
Mar 26, 2013
Posts
17
Reaction score
5
Ndugu zangu haswa wale waelewa ,akili iliyoshindwa kujitambua ni mzigo kwa maendeleo ya watu na taifa .kwa kuwa akili angavu ni
chimbuko la asili zenye kuleta mapinduzi ya ndani ya nafsi yenye matumaini ya maisha ya kijamii.

Mapinduzi ya nafsi yanaondoa utumwa wa kukubali kuonewa / kunyonywa /kudharauliwa na kupuuzwa huku ukishangilia ujinga na
kuukataa ujanja .watanzania wanahitaji mabadiliko na hakuna mabadiliko ya kweli yanayoweza kuletwa pasipokuwa na mapinduzi ya fikra.

Ni wajibu usioepukika kama vijana kuacha upumbavu ,tuepuke hila na udanganyifu .uoga tuuweke pembeni .tusiwe wachovu wa akili kwa kushindwa kufikiri .tusiweke tamaa na uchu mbele. Tusikubali kunyenyekea ,udhalimu na udhalilishwaji .kwa pamoja tupinge kwa
nguvu zote uonevu na umamluki .

Kwangu mimi masikini anayekula jasho lake ni bora kuliko jambazi anayeishi kwa kunyonya wenzake kama kupe. .ni heri kuwa na
waadilifu wachache kuliko wezi wengi. Binadamu yeyote anaweza kuwa na hasira. Lakini kuelekeza hasira zako kwa watu sahihi kwa kiwango sahihi ,kwa wakati sahihi na kwa njia sahihi si sifa ambayo kila mwanadamu anayo .

Nawapa elimu , elimu ya watu wazima ni kujifunza jambo ambalo litatusaidia kubadili na ku2umia mazingira hayo ili kuinua maisha yetu.
 
Back
Top Bottom