KipimaPembe
JF-Expert Member
- Aug 5, 2007
- 1,285
- 696
Katika jamii hii au iwe ni nchi yenye serikali yake, kuna mambo yafuatayo;
1. Hakuna kuoa wala kuolewa; mwanamke au mwanaume anaweza akatembea na anayemtaka ikiwa mmekubaliana. Mnaweza hata kuishi pamoja, ila ndoa hakuna na haitakiwi. Siku mkiboana kwa heri ya kuonana.
2. Mwanamke anaweza kuzaa na mwanaume yeyote provided ameridhia iwe hivyo. Si lazima mwanamke azae, akiamua kuzaa, analipwa posho ya uzazi mpaka takapojifungua. Kuna kodi ya kuendeleza jamii ambayo itaanzisha mfuko wa kulipa posho wanawake wanaoamua kuzaa.
3. Kulea watoto ni kazi ya serikali na kuna kodi ya kulea watoto ambayo watu wote hulipa, kama vile VAT. Mtoto akizaliwa, anapelekwa child care moja kwa moja ambapo malezi yanatolewa na watalaam haswa wa kulea watoto.
4. Maziwa ya mama ni biashara. Mama anaweza kwenda kunyonyesha kwenye kituo chochote cha kulea watoto na ni ruksa kunyonyesha mtoto yeyote ila hulipwa kwa kila mtoto anayenyonya na kushiba. Mf. Sh. 10,000 kwa mtoto.
5. Mzazi hatakiwi kujenga bond na mtoto wake. Kila mtoto ni mali ya jamii nzima hivyo hakuna cha huyu ni ndugu yangu.
6. Kutoka vituoni kwao watoto ni pale wanapopata ajira na kujitegemea (wanapofikia umri wa kufanya kazi). Watoto woote wanasoma hadi uwezo wao unapofikia.
Jamii ya namna hiyo nadhani inawezekana, na itaondoa hizi vurugu mechi na balaa za kila siku kwenye ndoa. Wanaume watakuwa responsible zaidi kwani wote ni bachelors. Kumwin mwanamke na kula itakuwa ni juu yao. Wanawake watakuwa na uhuru zaidi kwani woote wanajitegemea na hatutahitaji hizi feminism movement. Hakuna family strings!
Mnaonaje wanabodi jamii ya namna hiyo? Kwa nini tusifikirie kwenda huko?
kwanza wapo watakadandia/wa kuzidi kuku kutokana na haiba zao,
pili nchi itajaa within no time kwani kuna watakaoamua kuzaa mara tatu kwa mwaka,
tatu kuna wanaume/wake ambao itakula kwao kwani hawatapata kitu kabsaaa...waangalie mbwa wale wenye udhaifu huwa wanaishia tu kuwa kwenye kundi lakini hawapati kitu(!?)
nne kuna watakao nunua kina mama wawafanye kama hiace, kwani ukipata watatu tu wanaonyonyesha kipato hakitatofautiana na mwenye hiace
tano nchi ya aina hii itafutika kwenye uso wa dunia baada ya muda si mrefu kwani wengi wataondoka kwa ukimwi!
Yote uliyoyaandika yapo nchini Uingereza sasa;
...Mbaya, mbaya, mbaya sana.... ni mfumo mbaya, wala haufai hata kuigwa! Nchini Uingereza wanatumia sana mfumo huo, na matokeo/madhara yake ni pale mtu anapofikia hali ya uzee/ukongwe unamkuta anaishi kiasi miaka 15-20 ya mwisho wa uhai wake bila ndugu, jamaa wala marafiki mpaka kifo kinapomchukua.
Hayo madhara uliyoeleza yanawapata hata wenye ndugu katika umri mkubwa. Wengi wanaishi peke yao, pamoja na kuwepo na ndugu. Na kibaya zaidi hakuna care for eldery na wengi wanafall victims wa mauaji ya wachawi. Halafu ikiwa mfumo wa kulea wazee ni bora, wanaoingia kwenye hizo care homes za wazee ni wachache kwani wengi wanakuwa na pensheni za kuwatosha kuajiri walezi.
Hiyo si sababu ya kusema huo mfumo ni mbaya.