Fikiria jamii hii ya kusadikika

KipimaPembe

JF-Expert Member
Aug 5, 2007
1,285
696
Katika jamii hii au iwe ni nchi yenye serikali yake, kuna mambo yafuatayo;

1. Hakuna kuoa wala kuolewa; mwanamke au mwanaume anaweza akatembea na anayemtaka ikiwa mmekubaliana. Mnaweza hata kuishi pamoja, ila ndoa hakuna na haitakiwi. Siku mkiboana kwa heri ya kuonana.

2. Mwanamke anaweza kuzaa na mwanaume yeyote provided ameridhia iwe hivyo. Si lazima mwanamke azae, akiamua kuzaa, analipwa posho ya uzazi mpaka takapojifungua. Kuna kodi ya kuendeleza jamii ambayo itaanzisha mfuko wa kulipa posho wanawake wanaoamua kuzaa.

3. Kulea watoto ni kazi ya serikali na kuna kodi ya kulea watoto ambayo watu wote hulipa, kama vile VAT. Mtoto akizaliwa, anapelekwa child care moja kwa moja ambapo malezi yanatolewa na watalaam haswa wa kulea watoto.

4. Maziwa ya mama ni biashara. Mama anaweza kwenda kunyonyesha kwenye kituo chochote cha kulea watoto na ni ruksa kunyonyesha mtoto yeyote ila hulipwa kwa kila mtoto anayenyonya na kushiba. Mf. Sh. 10,000 kwa mtoto.

5. Mzazi hatakiwi kujenga bond na mtoto wake. Kila mtoto ni mali ya jamii nzima hivyo hakuna cha huyu ni ndugu yangu.

6. Kutoka vituoni kwao watoto ni pale wanapopata ajira na kujitegemea (wanapofikia umri wa kufanya kazi). Watoto woote wanasoma hadi uwezo wao unapofikia.

Jamii ya namna hiyo nadhani inawezekana, na itaondoa hizi vurugu mechi na balaa za kila siku kwenye ndoa. Wanaume watakuwa responsible zaidi kwani wote ni bachelors. Kumwin mwanamke na kula itakuwa ni juu yao. Wanawake watakuwa na uhuru zaidi kwani woote wanajitegemea na hatutahitaji hizi feminism movement. Hakuna family strings!

Mnaonaje wanabodi jamii ya namna hiyo? Kwa nini tusifikirie kwenda huko?
 
Wazazi wetu wametuachia mfumo wa kuishi kwa ndoa na kujenga familia ambomo watoto hupata malezi. Laikini ndoa leo zimekuwa chungu na shubiri hasa. Kwa nini tusirekebishe mambo haya? tuna maarifa na utaalamu zaidi.
 
kwanza wapo watakadandia/wa kuzidi kuku kutokana na haiba zao,
pili nchi itajaa within no time kwani kuna watakaoamua kuzaa mara tatu kwa mwaka,
tatu kuna wanaume/wake ambao itakula kwao kwani hawatapata kitu kabsaaa...waangalie mbwa wale wenye udhaifu huwa wanaishia tu kuwa kwenye kundi lakini hawapati kitu(!?)
nne kuna watakao nunua kina mama wawafanye kama hiace, kwani ukipata watatu tu wanaonyonyesha kipato hakitatofautiana na mwenye hiace
tano nchi ya aina hii itafutika kwenye uso wa dunia baada ya muda si mrefu kwani wengi wataondoka kwa ukimwi!
 
Yote uliyoyaandika yapo nchini Uingereza sasa;

Katika jamii hii au iwe ni nchi yenye serikali yake, kuna mambo yafuatayo;

1. Hakuna kuoa wala kuolewa; mwanamke au mwanaume anaweza akatembea na anayemtaka ikiwa mmekubaliana. Mnaweza hata kuishi pamoja, ila ndoa hakuna na haitakiwi. Siku mkiboana kwa heri ya kuonana.

...mambo ya civil partnership, au same sex parenthood

2. Mwanamke anaweza kuzaa na mwanaume yeyote provided ameridhia iwe hivyo. Si lazima mwanamke azae, akiamua kuzaa, analipwa posho ya uzazi mpaka takapojifungua. Kuna kodi ya kuendeleza jamii ambayo itaanzisha mfuko wa kulipa posho wanawake wanaoamua kuzaa.

...ni sawa na single parenthood, mama mmoja kila mtoto na baba yake, au baba mmoja kila mtoto na mama yake...

3. Kulea watoto ni kazi ya serikali na kuna kodi ya kulea watoto ambayo watu wote hulipa, kama vile VAT. Mtoto akizaliwa, anapelekwa child care moja kwa moja ambapo malezi yanatolewa na watalaam haswa wa kulea watoto.

...mfano wake kama fostering, adoption

4. Maziwa ya mama ni biashara. Mama anaweza kwenda kunyonyesha kwenye kituo chochote cha kulea watoto na ni ruksa kunyonyesha mtoto yeyote ila hulipwa kwa kila mtoto anayenyonya na kushiba. Mf. Sh. 10,000 kwa mtoto.

?

5. Mzazi hatakiwi kujenga bond na mtoto wake. Kila mtoto ni mali ya jamii nzima hivyo hakuna cha huyu ni ndugu yangu.

...mfano wake NSPCC , ambako ukimfinya mtoto wako mwenyewe, hawa jamaa watakuonyesha mtoto ni mali ya nani. kwa maelezo zaidi ingia hapa; [ame=http://en.wikipedia.org/wiki/NSPCC]NSPCC - Wikipedia, the free encyclopedia[/ame]

6. Kutoka vituoni kwao watoto ni pale wanapopata ajira na kujitegemea (wanapofikia umri wa kufanya kazi). Watoto woote wanasoma hadi uwezo wao unapofikia.

Jamii ya namna hiyo nadhani inawezekana, na itaondoa hizi vurugu mechi na balaa za kila siku kwenye ndoa. Wanaume watakuwa responsible zaidi kwani wote ni bachelors. Kumwin mwanamke na kula itakuwa ni juu yao. Wanawake watakuwa na uhuru zaidi kwani woote wanajitegemea na hatutahitaji hizi feminism movement. Hakuna family strings!

...unaishia Care homes for the elderly, kwa maelezo zaidi soma Care Home & Nursing Home, UK â€" elderly care homes

Mnaonaje wanabodi jamii ya namna hiyo? Kwa nini tusifikirie kwenda huko?

...Mbaya, mbaya, mbaya sana.... ni mfumo mbaya, wala haufai hata kuigwa! Nchini Uingereza wanatumia sana mfumo huo, na matokeo/madhara yake ni pale mtu anapofikia hali ya uzee/ukongwe unamkuta anaishi kiasi miaka 15-20 ya mwisho wa uhai wake bila ndugu, jamaa wala marafiki mpaka kifo kinapomchukua.
 
kwanza wapo watakadandia/wa kuzidi kuku kutokana na haiba zao,
pili nchi itajaa within no time kwani kuna watakaoamua kuzaa mara tatu kwa mwaka,
tatu kuna wanaume/wake ambao itakula kwao kwani hawatapata kitu kabsaaa...waangalie mbwa wale wenye udhaifu huwa wanaishia tu kuwa kwenye kundi lakini hawapati kitu(!?)
nne kuna watakao nunua kina mama wawafanye kama hiace, kwani ukipata watatu tu wanaonyonyesha kipato hakitatofautiana na mwenye hiace
tano nchi ya aina hii itafutika kwenye uso wa dunia baada ya muda si mrefu kwani wengi wataondoka kwa ukimwi!

kwanza jibu ni sheria ya kuzuia wanawake kuzaa sana. Mf. mwanamke mmoja haruhusiwi kuzaa more than once katika miaka mitano. Pili si salama kwa mwanamke kuzaa zaidi ya mara nne in life time, hivyo akizaa mara ya nne, funga kizazi.

Pili, Haiwezekani kuzaa mara tatu kwa mwaka na wanawake wengi hawependi kuzaa zaa ovyo.

Tatu, hadi leo wapo ambao hawapati, kuna wanaume wanaaibu ya kutongoza. Kuna wanawake ni mahunde kwelikweli hawatongozwi.

Nne, wakati hakuna ndoa nani atakayewafanya dala dala. Watoto wa kunyonyeshwa wakiwa wachache, kunyonyesha kwa tenda. Mwenye bei nafuu.

Tano, ukimwi haudhibitiwi na ndoa. Leo wenye ndoa ndo wengi wana ukimwi. Maana yake ni kuwa wenye ndoa ndo hufanya mapenzi yasiyo salama zaidi.
 
Yote uliyoyaandika yapo nchini Uingereza sasa;

...Mbaya, mbaya, mbaya sana.... ni mfumo mbaya, wala haufai hata kuigwa! Nchini Uingereza wanatumia sana mfumo huo, na matokeo/madhara yake ni pale mtu anapofikia hali ya uzee/ukongwe unamkuta anaishi kiasi miaka 15-20 ya mwisho wa uhai wake bila ndugu, jamaa wala marafiki mpaka kifo kinapomchukua.

Hayo madhara uliyoeleza yanawapata hata wenye ndugu katika umri mkubwa. Wengi wanaishi peke yao, pamoja na kuwepo na ndugu. Na kibaya zaidi hakuna care for eldery na wengi wanafall victims wa mauaji ya wachawi. Halafu ikiwa mfumo wa kulea wazee ni bora, wanaoingia kwenye hizo care homes za wazee ni wachache kwani wengi wanakuwa na pensheni za kuwatosha kuajiri walezi.

Hiyo si sababu ya kusema huo mfumo ni mbaya.
 
...pensheni ya kutosha kuajiri walezi! ...si yale yale tu?

Anyway, binafsi na kwa maoni yangu huo ni mfumo mbaya. Kama wewe umeupendelea, kila la kheri.
 
Kama mfumo huo sadikika una practice huko Uingereza, ni sawa. Lakini kwa Africa ni ngumu sana kwa sababu zifutazo;
1. Waafrika wanw wivu sana, hawawezi kushea na mwenzake
2. Ukimwi umeshika hatamu Africa
3. Kuna watu watashindia kazi hiyo ya ngono tu, coz people are very lazy
4. Watu wanapenda visasi sana,
 
Nchi kama hiyo ina maana kila mwananchi Mungu wake ni Serikali - katika maisha ya mwanadamu lifestyle ya mtu inategemea sana na imani yake kwa Mungu. Wanaomhofu Mungu wanakuwa na maadili mema kama mawakili wa Mungu - na wanaompenda ibilisi hufanya kama baba yao Ibilisi - mfano - vitabu vitakatifu vinapinga sana ngono holela na wanaomhofu Mungu ndio wanatekeleza hili - kwani ngono nje ya ndoa ni dhambi - na unapofanya hata kama ni sirini - Mungu anakuona - so you do things respecting your creator.
 
1. Wivu vipi? Mwanadamu inherently ana asili ya wivu! Yaani zitapigwa na kesi kila siku!!!

2. Sura, umbo na urembo: je wale akina dada wenye maumbo sura isiyovutia vipi? hapa wanaume watauana kupigania walio warembo zaidi!

3. Kazi: incentives za kufanya kazi kutokuwa hakuna maana hakuna family responsibilities na competition..maendeleo yatarudi nyuma!

Hii ibaki tu ktk kufikirika.. as human beings are not animals!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom