Siasa ni itikadi siyo ugomvi, chuki na uhasama. Itikadi ndio zinatofautisha chama kimoja na kingine au wanachama. Kupitia Itikadi za vyama wananchi wanaunganishwa na sera madhubuti za maendeleo kutoka chama husika. Hivyo tofauti zetu tuwe tunaziweka pembeni kama huyo kuku anavyomlea bata kwa ajili ya maslahi mapana ya nchi yetu.