FIFA yaifungia Nigeria

Mphamvu

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2011
Posts
10,702
Reaction score
3,356
Shirikisho la soka duniani FIFA, limeisimamisha kwa muda timu ya Taifa ya Nigeria kushiriki katika mashindano ya Kimataifa kutokana na Serikali ya nchi hiyo kuingilia kati michezo ya timu hiyo kinyume cha sheria na taratibu za FIFA kwa nchi wanachama.

Uamuzi huo ulifanyika Jumatatu baada ya wajumbe kadhaa wa shirikisho la soka la Nigeria (NFF) kufikishwa mahakamani.

"...wakati wa kusimamishwa kwa muda, shirikisho la NFF halitawakilishwa kwenye mashindano ya kanda, bara Afrika au kimataifa, pamoja na mechi za kirafiki," taarifa hiyo ya FIFA ilisema.

Kufuatia marufuku hii, hatma ya mechi ya wikiendi hii ya Nigeira dhidi ya Guinea mjini Conakry haijulikani.

Chanzo: Hatimaye FIFA yaifungia Nigeria - wavuti.weebly.com
 
Mbona serikali hizohizo zinapolipa mishahara ya makocha, kulipa posho za wachezaji baada ya za FIFA kuliwa na hao wanaoondolewa na Serikali, FIFA huwa haizifungii hizo nchi (wala walaji wa hizo fedha?). Kwani kuingilia si kuingilia tu?
 
Nadhani wanalenga kuingilia ambako kuna madhara hasi...
 
Stupid FIFA, Dawa ya FIFA inapikwa. Haivumiliki FIFA kuwa sovereign over national governments! France is initiating this move!
 
Nadhani wanalenga kuingilia ambako kuna madhara hasi...
Huko ni kukubali kunywa mchuzi, lakini nyama ya mchuzini usile. Au utekelezaji wa ule usemi 'Baniani Mbaya, Kiatu chake dawa.' Madhara hasi hufanywa zaidi na FA husika kwa kuongoza kitapeli na kuwanyima wachezaji posho zao. Ningewaelewa FIFA kama wangekuwa wakali kwa FA za aina hiyo kama walivyo wakali kwa Serikali hizo zenye madhara hasi. Madudu ni madudu tu, bila ya kujali nani anayeyafanya.
 
Stupid FIFA, Dawa ya FIFA inapikwa. Haivumiliki FIFA kuwa sovereign over national governments! France is initiating this move!

mkuu hebu ninyonyee hii muvu wanataka kuanzisha shirikisho mbadala au
 
Mambo ya posho yako huku kwetu tu. FIFA wanazo organ zao za kinidhamu, ya juu kabisa ikiwa Mahakama ya Michezo, watu wenye mashtaka, mapingamizi n.k wanatakiwa waende huko.
 
mkuu hebu ninyonyee hii muvu wanataka kuanzisha shirikisho mbadala au

No, wanataka FIFA isiwe juu ya mamlaka ya nchi huru. Kuna tetesi inaweza kuwa kama ilivhyo ngumi, si unajua kuna makundi kibao ya world boxing associations! Wanakerwa sana na FIFA kuwa immutable, kujipa madaraka kuzidi mipaka, which is welcome
 
Mambo ya posho yako huku kwetu tu. FIFA wanazo organ zao za kinidhamu, ya juu kabisa ikiwa Mahakama ya Michezo, watu wenye mashtaka, mapingamizi n.k wanatakiwa waende huko.
Mtu umnyime posho yake, halafu akaidai kwenye Mahkama iliyoko dunia nyengine? Huo ndio urasimu unaosababisha yote hayo.
 
Mbona serikali hizohizo zinapolipa mishahara ya makocha, kulipa posho za wachezaji baada ya za FIFA kuliwa na hao wanaoondolewa na Serikali, FIFA huwa haizifungii hizo nchi (wala walaji wa hizo fedha?). Kwani kuingilia si kuingilia tu?
FIFA in kama genge la wahuni , halafu Blatter anawatetea sana hawa wabadhilifu wenzake Wa Afrika kwasababu ndio wanamweka madarakani .Kila Mara anapata kura zote Afrika bila kupingwa
 
FIFA in kama genge la wahuni , halafu Blatter anawatetea sana hawa wabadhilifu wenzake Wa Afrika kwasababu ndio wanamweka madarakani .Kila Mara anapata kura zote Afrika bila kupingwa
kama huwezi Ufisadi, huwezi kuwa mwana-FIFA. Ni kama genge la wachawi. Mwenzao akidondoka na ungo wakiwa safarini, wao wanamtelekeza. Angalia walivyomfanya Bin Hammam.
 
kama huwezi Ufisadi, huwezi kuwa mwana-FIFA. Ni kama genge la wachawi. Mwenzao akidondoka na ungo wakiwa safarini, wao wanamtelekeza. Angalia walivyomfanya Bin Hammam.

Naungana na wewe mkuu, ni genge la wahuni na kilichafanyika ni mwizi kumwibia mwizi. Nguvu ya fedha ya Bin Hamam ilikuwa inamtisha SB akaona amuwahi mapema.
 
Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…