Shirikisho la soka la kimataifa FIFA litamtuma afisa wake anajeshughulikia wanachama bwana Primo Corvaro
kuja nchini pamoja na ujumbe wake ili kusikiliza pande zote zinazohusika na mgogoro wa uchaguzi TFF ulioibuka baada
ya kuondolewa majina ya baadhi ya wagombea kwenye nafasi mbalimbali za uongozi wa TFF.
Uzoefu unaonyesha kwamba FIFA huwatumia maafisa wake kutoka katika idara ya sheria au idara ya wanachama iliyo chini ya mkurugenzi Thierry Regenass ambapo bwana Primo Corvaro ni meneja anayeshughulikia mahusiano ya wanachama wa FIFA pamoja na bwana Marco Leal kutoka idara ya sheria na Hadhi za wachezaji. Sambamba na hao FIFA pia katika kutatua migogoro huwatumia wajumbe waliopo kwenye kamati ya wanachama yaani Associations Committee ambapo Bw L Tenga ni mjumbe kutoka Afrika, wajumbe wengine kwenye kamati hiyo wanaotoka Afrika ni Adam Mthethwa kutoka Swazland, Kwesi Nyantakyi kutoka Ghana, Walter Nyamilandu kutoka Malawi, Hamidou Djibrilla kutoka Niger, na Makamu mwenyekiti wa kamati hiyo kutoka Algeria Bw Mohamedd Rouaroua, Mwenyekiti wa kamati hiyo ni bwana Erzik Senes wa Uturuki.
Ni matarajio ya wapenda soka wa Tanzania kwamba ujumbe wa FIFA utatenda haki kwa wote.